Prezzo anatarajia kupata mtoto wa pili

0
732

PREZZO (1)NAIROBI, Kenya

NYOTA wa muziki nchini Kenya, Jackson Makini ‘CMB Prezzo’ anatarajia mtoto wa kiume hivi karibuni.

Prezzo amempa jina la Gabriel mtoto huyo kabla hajazaliwa. Msanii huyo mpaka sasa hajaoa, lakini ana mtoto mmoja na sasa anatarajia kupata mtoto wa pili.

“Natarajia mtoto wa kiume siku yoyote, ni furaha kubwa kupata mtoto wa kiume kwa kuwa naamini ataiga mambo yangu mengi, ikiwemo aina ya mavazi ninayopenda kuvaa.

“Nimeamua kumpa jina mapema kabla ya kuzaliwa kwa kuwa najua jinsia yake, baada ya kufanya uchunguzi kwa madaktari,” alimaliza Prezzo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here