23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

MDEE KUPELEKA HOJA BUNGENI KUPINGA MASHARTI BODI YA MIKOPO

Na SALOME SAMWELI, TUDARCo

MWENYEKITI wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Halima Mdee, amesema watapeleka hoja Bungeni kupinga uamuzi wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kubagua utoaji wa mikopo kwa kisingizio cha watoto wa wanasiasa na viongozi waliojaza fomu za maadili kwa viongozi wa umma.

Wiki iliyopita Bodi hiyo ilitangaza masharti kumi kwa wanafunzi wanaotarajia kuomba ufadhili kwa mwaka wa masomo 2017/18 na wanaoendelea, mawili kati yake yanaeleza kundi la wanafunzi ambao hawastahili kuomba.

Katika taarifa ya HESLB, wanafunzi ambao wazazi wao ni wakurugenzi au mameneja waandamizi kwenye makampuni yanayotambuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), hawatatakiwa kuomba mikopo hiyo.

Aidha, watoto wa viongozi na wanasiasa waliosaini fomu za maadili kwa viongozi wa umma wasithubutu kuomba mikopo hiyo.

“Bodi ya Mikopo imekuja na hoja nyepesi zisizo na mantiki kwa kubagua wanafunzi kupata elimu. Diwani hana mshahara, lakini wamechukua kipengele cha yeye kubanwa na sheria kusaini fomu ya maadili na kumfananisha na wabunge wenye mishahara na kumnyima haki ya mwanawe kukopeshwa fedha,” alisema Mdee.

Mdee, ambaye ni Mbunge wa Kawe, alisema Waziri Kivuli wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi atatoa taarifa ya uchambuzi ni kwa njia gani wanafunzi wa Tanzania wananyimwa haki ya kikatiba ya kupata mikopo.

“Huu ni ubaguzi wa kielimu ambao ni kinyume na matakwa ya Katiba, tulitarajia serikali itakuwa mstari wa mbele kuhakikisha watu wake wanapata elimu na hasa mikopo, lakini vigezo hivi watoto wa madiwani hawataendelea na masomo kwa vile wazazi wao wanaonekana wana mishahara, jambo ambalo siyo kweli,” alifafanua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles