29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

MCHUNGAJI MSINGWA ANYOSHEA KIDOLE TAKUKURU  

 

Na MWANDISHI WETU-DODOMA


MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema hana mpango wa kupeleka ushahidi wa kununuliwa kwa madiwani wa jimbo lake katika taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

Msigwa ambaye Oktoba Mosi, mwaka huu aliambatana na wabunge wa chama hicho mkoani Arusha, Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) na Godbless Lema (Arusha Mjini), kwenda Ofisi ya Takukuru, kupeleka ushahidi unaowaonyesha wabunge wa Chadema wakishawishiwa kwa rushwa kuhamia Chadema.

Akizungumza jana na MTANZANIA, alisema alikuwa anasubiri kuona namna ushahidi uliowasilishwa na Nassari utakavyofanyiwa kazi ndipo apeleke wa kwake.

“Kwa jinsi Mkurugenzi wa Takukuru alivyolipeleka suala hili kwa kweli siwezi kumpelekea ushahidi wangu nitatafuta mbinu nyingine lakini Takukuru sina imani nayo.

“Ukiangalia mtuhumiwa mwenyewe ndiyo kwanza amepandishwa cheo, sasa kuna nini tena kama mtu anatuhumiwa kwa rushwa, uchunguzi haufanyiki unashangaa anapandishwa cheo anakuwa Mkuu wa  Mkoa,” alisema Msigwa.

Septemba mwaka huu, Nassari na Lema walidai kuwa na ushahidi uliomuonyesha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti akiwashawishi baadhi ya madiwani wa Chadema kwa rushwa ili wahamie Chama Cha Mapinduzi (CCM).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles