24.5 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

WABUNGE WAKUNWA NA UTENDAJI WA MAX MALIPO  

 

Na MWANDISHI WETU-DODOMA


WABUNGE wameishauri Serikali kuzipa kipaumbele kampuni za wazawa ikiwamo Kampuni ya Maxcom Africa PLC, maarufu Max Malipo na kudhibiti watendaji wachache walioanza kuiwekea vikwazo ili kuinyang’anya huduma kampuni hiyo.

Wakizungumza katika semina ya kuelezea mchakato wa kuanza kuuza hisa za kampuni Soko la Hisa na Mitaji Dar es Dar Salaam (DSE) ambapo inategemea kupata Sh bilioni 22 kwenye mauzo hayo, wabunge walisema fedha inazopata kampuni hiyo zitabaki nchini kwa sababu inamilikiwa kwa asilimia 100 na Watanzania wazawa pamoja kutoa ajira.

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) aliitaka Serikali kuacha tabia ya kuwaondoa wazawa waliowekeza nchini ikiwamo Tume ya Sayansi  na Teknolojia (Costech).

Alisema Maxcom akikua atalipa kodi zote, atataoa ajira kwa Watanzania na pia mzunguko wa fedha utabaki nchini.

“Serikali ikizidi kufanya hayo tutapata hasara kwa sababu ninyi hamlipi kodi ya ongezeko la thamani (VAT), kodi ya makampuni lakini pia hamfanyi biashara.

“Sasa kwa nini Serikali inatenga fedha kufadhili miradi ya teknolojia ya mawasiliano kama hii pale Costech kama kila zao linalotoka hapo tunaliondolea mradi kwa sababu imepata mradi mkubwa, yaani vijana wametengeneza ubunifu wao kwa miaka sita hadi saba wanafika mahali wakubwa wanawanyang’anya wanaleta watu wengine.

“Mimi nilikuwa naiomba serikali isiwaonee wivu Watanzania katika kupata fedha, aliyewahi kulichungulia dili akalipata mwachieni,” alisema Bashe.

Mbunge wa Ileje, Janeth Mbene (CCM), alisema anasikitika kampuni hiyo kupigwa vita na idara za Serikali kwani amesikia wamenyang’anywa baadhi ya huduma.

“Kama TRA, kama kuna sehemu wamekosea warekebishwe na si kunyang’anywa, maadui lazima wawepo sasa tusirudi nyuma, tusiingize vitu binafsi kwenye maslahi ya taifa, vitu hivi vinawakimbiza vijana nje,” alisema.

Mbunge wa Singida Magharibi,  Elibariki Kingu (CCM), alisema inashangaza Serikali inawezekeza fedha kuibua vipaji vya Watanzania halafu wanakuwa wakubwa na kuanzisha kampuni ndipo baadhi ya watendaji wanawaua.

Akizungumzia mauzo ya hisa, Mtendaji Mkuu wa Zan Securities ambao ni washauri wa masuala la hisa wa Maxcom, Raphael Masumbuko alisema Maxcom inatarajia kuuza asilimia 25 ya hisa zake kwenye soko la hisa na Mitaji Dar es Salaam na kupata Sh bilioni 22. Kwa sasa thamani ya kampuni hiyo ni Sh bilioni 68 hivyo baada ya mauzo ya hisa thamani itafikia Sh bilioni 90.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Jamson Kasati ambayo ni ya kwanza kutoa huduma za ununuzi wa LUKU kwa njia ya mtandao, alisema kwa siku kampuni hiyo inachakata miamala 600,000 huku uwezo wake kwa sasa ni kuchakata miamala milioni tano kwa siku.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles