23.5 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mchezaji Sunderland jela miaka sita

adam johnsonLONDON, England

ALIYEKUWA winga wa timu ya Sunderland, Adam Johnson, amehukumiwa miaka sita jela kwa kukutwa na kosa la kufanya vitendo vilivyokuwa vikiashiria ngono  na  msichana wa miaka 15.

Johnson  alikamatwa tangu Machi 2 mwaka jana kwa kosa la kujihusisha na vitendo vilivyokuwa vikiashiria ngono akiwa na msichana wa miaka 15.

Akiwa katika mahojiano mbele ya polisi, Johnson alikiri kumbusu msichana huyo baada ya kuwa katika mipango ya kukutana naye kwenye gari lake aina ya Range Rover, huku akimuahidi kumsainia jezi ya Sunderland.

Mchezaji huyo alikutwa na hatia Machi 2, mwaka huu, katika mahakama ya Bradford Crown iliyopo Bradford, England.

Kiungo huyo wa Sunderland mwenye umri wa miaka 28, mkazi wa Castle Eden, mji wa Durham, England, alikuwa na mashitaka mawili yaliyokuwa yakimuandama, likiwamo la kujihusisha na vitendo vya ngono akiwa na msichana mdogo na kuwa na tabia ya kuongopa ili kuwalaghai wasichana wadogo.

Hata hivyo, mchezaji huyo alidhani angeepuka hukumu hiyo kutokana na dhana ya kuwa maarufu wakati  kesi hiyo ikisikilizwa siku ya Alhamisi, kabla ya kutolewa hukumu.

Mahakama  hiyo ilielezwa  na mtaalamu wa akili kwamba Johnson alivurugwa  kutokana na kusababisha  kutojitambua kama alikuwa mchezaji wa soka England.

Mtaalamu huyo alisema kuwa mchezaji  huyo alidhani angeweza kufanya ngono na msichana yeyote alipotaka na kwenda zake na kutumia vibaya nafasi yake ya kuwa mchezaji wa Ligi Kuu na timu ya taifa.

Hakimu wa kesi hiyo, Jonathan Rose, alisema kwamba Johnson alikuwa na uwezo wa kujizuia kutofanya vitendo hivyo kutokana nafasi yake ya heshima akiwa Sunderland.

Lakini  Johnson alikiri kuongozwa na maisha ya kudhania kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya kila kitu, ambapo wataalamu walidai kwamba alidumaa kwa kujiona bado mdogo kiakili.

Kwa sasa mama na baba yake wamemwacha akiwa mwenyewe jela na kujikuta akiwa mpweke, akiwa amepoteza kila kitu kwenye  maisha ya soka, ikiwamo kazi, mchumba na mtoto wake.

Nyota huyo halishindwa kufahamu kuwa  mpira haupo  juu ya sheria ambapo Johnson itambidi kulagharamikia ili kugundua  jambo hilo.

Hata hivyo, Johnson  alijikuta akimdanganya mpenzi wake, Stacey Flounders baada ya kufanya vitendo hivyo na shabiki wake  wa soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles