32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, February 5, 2023

Contact us: [email protected]

Ramos nje kikosi cha Hispania dhidi ya Romania

RamosMADRID, Hispania

MCHEZAJI wa timu ya taifa ya Hispania na Real Madrid, Sergio Ramos, anatarajia kukosa mchezo wa kimataifa dhidi ya Romania utakaochezwa Jumanne hii, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti aliyopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.

Beki na nahodha huyo wa timu ya Madrid alilazimika kutolewa  nje  kipindi cha kwanza kutokana na maumivu hayo na kushuhudia  timu yake ikitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Italia.

Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Hispania (FA), mchezaji huyo ameondoka kwenye kambi ya timu hiyo Ijumaa iliyopita kutokana na majeraha hayo.

Beki huyo wa kati alilazimika kuondolewa kwenye kambi hiyo na kurudi Hispania kwa uchunguzi zaidi, huku timu hiyo ikiendelea kujiandaa kuvaana na Romania.

Hata hivyo, Madrid itakuwa na hamu ya kuona beki huyo anarejea uwanjani mapema akiwa yupo fiti kabla ya mchezo wao wa El Clasico dhidi ya Barcelona, utakaochezwa Jumamosi ijayo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles