24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

MCHAKATO WAANZA MOSHI KUWA JIJI

Na  Upendo Mosha, Moshi


SERIKALI mkoani Kilimanjaro, imewataka madiwani wa halmashauri za wilaya ya Hai na Moshi kuacha ubinafsi  katika upanuzi wa mji wa Moshi kuwa jiji.

Badala yake, madiwani hao wametakiwa kushirikiana kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa mchakato huo.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, alitoa agizo hilo jana, wakati  wa kikao cha uzinduzi wa kutangazwa kwa upanuzi wa mpaka wa kiutawala  na utayarishaji wa mpango kabambe wa mjini wa Moshi.

Alisema baadhi ya madiwani wa halmashauri za wilaya ya Moshi na Hai, wamekuwa na tabia ya kuendekeza ubinafsi katika upanuzi wa mji huo, jambo ambalo limekuwa likisababisha kukwamisha lengo hilo.

Alisema  suala la ubinafsi, limekuwa likirudisha nyuma

maendeleo ya  wananchi wa wilaya hizo.

“Madiwani wa halmashauri za  Moshi na Hai, muwe wazalendo embu acheni tabia za ubinafsi upanuzi wa mji wa Moshi ni la manufaa kwetu wote, ninawataka mshirikiane kwenda kwa wananchi kutoa elimu sahihi juu ya

umuhimu wa mchakato huu”alisema

Alisema na kuongeza wapo baadhi ya viongozi wa kisiasa ambao

wamewatangazia wananchi  eti hawakushirikishwa.

“Ni jambo la kushangaza,wapo wanasiasa wanatoka hapa na kwenda kwa wananchi kupandikiza chuku,uongo na majungu hawakushirikishwa, mchakato huu ulishirikisha viongozi wa

pande zote mbili,” alisema

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Mipango Mji  na Ardhi wa Manspaa ya Moshi, Uhuru Mwembe alisema hakuna mwananchi atakaye ondolewa katika eneo lake.

Diwani wa Kata ya Mawenzi,Hawa Mushi, aliziomba baadhi ya taasisi za umma,ikiwamo Wakala wa Barabara Tanroads) na mamlaka za maji kutoa ushirikiano katika

upanuzi huo.

Tayari tangazo la Serikali (GN)  namba 219 la kuridhia mapendekezo ya kuongeza mipaka ya utawala ya manispaa ya Moshi kutoka kilomita  za mraba 58 hadi 142 ambapo zitamegwa kilomita za mraba 68 halmashauri

ya Moshi Vijijini na kilomita za mraba 16  kutoka Wilaya ya Hai,

limetolewa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles