Na MWandishin wetu |
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amemuomba Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla kufanya utaratibu wa kuwarudishia silaha aina ya Magobole zilizochukuliwa na serikali wakati wa oparesheni tokomeza ujangili.
Mbunge huyo ametoa ombi hilo kutokana na wananchi kulalamika, kuchukuliwa silaha zao na serikali na mpaka sasa hazijarudishwa.
Muheshimiwa waziri kwa wazee wa Kiziguwa, Gobole ni heshima kule kwetu hivyo naomba kwa wale ambao hawajabainika kujihusisha na matumizi mabaya ya silaha hizo warudishiwe”, alisema Ridhiwani.
Ameendelea kubainisha kwamba wapo wananchi wema na wengine sio wema hivyo serikali itazame namna bora ya kuzirudisha silaha hizo maana malalamiko kutoka kwa wananchi ni mengi kuhusiana na serikali kuwanyang’anya magobole hayo.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangwalla amesema serikali inatambua kwamba wapo wananchi ambao wanazitumia silaha hizo vibaya kwa kufanya ujangili hivyo watalishughulikia kwa mujibu wa utaratibu.