26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Sanga aipigia magoti Serikali kusuasua shamba la ng’ombe

Na Mwandishi Wetu, Makete

Mbunge wa Makete, Festo Sanga, ameiomba serikali kuligeukia shamba la Maaalum la kitulo la Ng’ombe wa maziwa ambalo lilianzishwa na Hayati Baba wa Taifa, Julias Nyerere, kwa ajili ya kuzalisha maziwa kwa ajili ya Viwanda vya Tanzania na Watanzania.

Shamba la Kitulo ndio Shamba pekee kwa ukanda wa Afrika Mashariki lenye ng’ombe wanaotoa lita 40-50 kwa siku, lakini kwa muda mrefu limekuwa halikui na ng’ombe hawaongezeki.

Sanga ambaye alifanya ziara ya kukagua shamba hilo leo Machi 9, amemuomba, Rais na Wizara husika kuchukua hatua za Maksudi kuhakikisha shamba hili linakuwa na tija ambayo Nyerere aliiona, hasa ikiwa ni kuzalisha maziwa ya kutosha kwa Watanzania wote.

“Kwa sasa Shamba halina vifaa vya kisasa vya kuendeshea shughuli za shamba, lakini majengo ni chakavu, na idadi ya mifugo imekuwa ikipungua badala ya kuongezeka,” amesema Sanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles