25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

“Bila ya Mwanamke kupewa nafasi ni ngumu kufikia usawa”- Masanja

Na Derick Milton, Simiyu

Imeelezwa kuwa ili kuweza kufikia dunia yenye usawa wa kijinsia, ni lazima mwanamke aweze nafasi ya kupatkushika atamu ya uongozi kwenye jamii na kuondoa dhana kuwa kiongozi bora lazima awe mwanaume.

Hayo yamesemwa leo na Mratibu wa mradi wa Shishiyu Maswa kutoka Shirika la World Vision Tanzania Yohana Masanja, wakati wa maamizishimo ya siku ya wanawake mkoa wa Simiyu yaliyofanyika Wilayani Maswa kimkoa.

Masanja amesema kuwa ikiwa jamii itashindwa kubadilika na kutambua kuwa kiongozi bora anaweza kuwa mwanamke pia kama ambavyo ilivyo kwa mwanaume, lile lengo la kufikia dunia yenye usawa haliwezi kufikiwa.

Amesema kuwa maeneo mengi ambako wanawake wamekuwa na uwezo na kupata nafasi ya uongozi, maendeleo makubwa yameonekana na kuwepo kwa ufanisi wa kutosha.

“Mfano ikiwa mwanamke kwenye ngazi ya familia aikiwa na uwezo wa kushika atamu, watoto watakuwa na ustawi, tofauti ikiwa mwanaume ndiye atakuwa na uwezo, watoto hawawezi kuwa na ustawi,” amesema Masanja.

Mratibu huyo amesema kuwa elimu bado inahitajika kwa kiwango kikubwa ili kubadilisha jamii na kutambua mchango wa mwanamke katika kuleta maendeleo ya taifa au familia yeyote ni mkubwa na unahitajika.

Aidha amesema kuwa Shirika la Worldvison limeendelea kutekeleza miradi mbalimbali, ambayo imekuwa ikilenga kumwezesha mwanamke kiuchumi, kijamii na kisiasa ikiwa pamoja na kupiga vita mimba za utotoni.

Kwa upande wake Mratibu wa Afya na Lishe kutoka Shirika hilo Kanda ya Nzega Dkt. Kaserwa Stanford, amesema kuwa ili kuweza kupambana na tatizo la lishe duni katika jamii lazima wanawake wapewe elimu ya lishe bora.

Dkt Stanford ameongeza kuwa wanawake ndiyo wenye uwezo wa kuhakikisha tatizo la lishe duni kwenye jamii linaisha, ikiwa watapewa elimu ya uandaaji wa vyakula kwa watoto wao tangu wakiwa wachanga hadi wanakua.

Baadhi ya wanafunzi walioshiriki maazimisho hayo wamesema kuwa tatizo kubwa ambalo linachangia wasichana kupata mimba ni tama pamoja na kukosa elimu ya uzazi.

“Wanafunzi wengi hasa wa kike wamekuwa na tama, lakini wengine elimu ya uzazi hawana, ndiyo maana wamekuwa wakijikuta wanapata ujauzito na kukosa masomo kwa kufukuzwa shule au kuacha,” amesema Kresensia Kizinja Mwanafunzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles