33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanachama Wanawake(MCP) waadhimisha siku ya wanawake kwa harambee

Na Clara Matimo, Mwanza

Wanachama Wanawake kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza (MPC), wameadhimisha siku yao kwa kufanya harambee ili kupata fedha kwa ajili ya  kuanza ujenzi wa ofisi za chama hicho katika eneo la  Kata ya Bujashi Kijiji cha Matale  Wilayani Magu Mkoani Mwanza.

Diwani wa Kata ya Bujashi, Deleli Mazoya, (CCM),kulia akimkabidhi Katibu Msaidizi wa MPC, Blandina Chagula, (kushoto) kibali cha ujenzi wa jengo la ofisi ya Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza katika Kijiji cha Matale  Wilayani Magu huku baadhi yawaandishipamoja na viongozi waSerikali ya kijiji wakishuhudia.Picha na Clara Matimo.

Harambee hiyo imefanyika baada ya  waandishi hao kutembelea eneo hilo na kukabidhiwa hati miliki, kibali cha ujenzi na ramani ya jengo hilo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Uendeshaji Ardhi ya Landspecs Developers, Ally Msoya, ambayo imeingia ubia wa kupima na kuuza viwanja  vilivyopo kijijini hapo na halmashauri ya Wilaya ya Magu.

Msoya ambaye aliambatana na Diwani wa Kata ya Bujashi, Deleli Mazoya, (CCM), Diwani wa Kata jirani ya Bukandwe, Marco Minzi, pamoja  na baadhi ya viongozi wa Serikali ya  Kijiji hicho aliichangia MPC mifuko 50 ya saruji huku viongozi hao wakichangia mifuko mitano kila mmoja .

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kibali cha ujenzi katika eneo hilo na Diwani Mazoya, Katibu Msaidizi wa MPC, Blandina Chagula, alisema jengo hilo la ghorofa tatu likikamilika litatoa  fursa kwa wananchi ambao watapanga vyumba kwa ajili ya kufanya biashara  hivyo watajikwamua kiuchumi.

“Pia jengo likikamilika MPC tutapata faida kubwa sana kwa sababu litatuongezea kipato kutokana na wapangaji watakaopanga kwetu, fedha hizo zitatusaidia kuanzisha miradi mingine ambayo itatuinua kiuchumi na kutufanya tuheshimike zaidi ndani ya jamiilakini kubwa zaidi tutaondokana nakudaiwa kodi yapango la ofisi kama ambavyo tunapanga sasa,”alisema.

Baadhi ya wanachama wa MPC, akiwemo Kisali Simba na Rose Jacob, walisema waliamua kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kuhakikisha wanafanya jambo ambalo litakumbukwa endapo jengo hilo likikamilika ndiyo maana wakaona wafanye harambee ili kupata vifaa vya ujenzi.

“Tunamshukuru Mungu sana wazo letu limeleta matokeo chanya, harambee tumeifanyia eneo hili  tena hatujaalika watu wengi zaidi ya viongozi wa eneo hili lakini tumefanikiwa kupata mifuko mingi ya saruji,mchanga na kokoto, kwetu sisi ni faraja, kweli  wanawake tunaweza na leo ni mwanzo tutaandaa harambee nyingine ambayo itawashirikisha wadau wetu wengi,”alisema Kisali.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko,  alisema kitendo kilichofanywa na wanachama hao kimethibitisha  kwamba wanawake wanauwezo wa kusimamia msingi wa kujitegemea kwa sababu wamefanikisha upatikanaji wa mifuko 100 ya saruji ambayo itasaidia kuanza kwa ujenzi wa jengo hilo.

“Wito wangu kwa taasisi zote za habari nchini msingi  wa waandishi wa habari usimamie katika kumheshimu mwanamke, tuone  mwanamke ana haki sawa na mwanaume  ndani ya  news room, tuone mwanamke  ana haki sawa katika ufanyaji wa kazi,  tutoe ubaguzi na wanaume tuonyeshe mfano, moja ya malengo ya MPC ni kusimamia usawa wa kijinsia na hilo tunalitekeleza  kwa vitendo,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles