27.9 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Mathayo kuwawezesha wananchi kiuchumi

Na Shomari Binda,Musoma

Mbunge wa Musoma mjini, Vedastus Mathayo amesema kipindi hiki cha miaka mitano (2020-2025) amedhamiria kuwatumikia zaidi wananchi kwa kuwawezesha kiuchumi.

Akizungumza na MtanzaniaDigital leo Januari 7, katika mahojiano maalum, Mathayo amesema licha ya shughuli nyingine za kijamii lakini suala la uchumi wa wananchi litapewa kipaumbele.

Amesema wananchi watafikiwa na kuwezeshwa kiuchumi kupitia fedha zinazotolewa na halmashauri pamoja na mfuko maalum atakaouanzisha.

Mathayo amesema katika kipindi cha kampeni moja ya ahadi alizotoa ni kuwawezesha wananchi kiuchumi na kilichobaki ni utekelezaji huku akiwataka wananchi ambao bado hawajajiunga kwenye vikundi kufanya hivyo ili iwe rahisi kufikiwa.

“Katika kipindi hiki cha miaka mitano moja ya mambo nitakayoyapa kipaumbele ni uchumi wa wananchi kupitia mikopo isiyo na riba kubwa ili wafanye shughuli za ujasiliamali.

“Kabla ya kuwawezesha wananchi kwanza watapatiwa mafunzo kupitia wataalam ili waweze kufanya kazi zao bila kupata hasara.

“Mwananchi anapokuwa na fedha anawezq kuchangia shughuli za maendeleo zikiwemo za elimu kwa kuchangia ujenzi wa madarasa,” amesema Mathayo.

Aidha, amewaomba madiwani katika kata zote 16 za jimbo la Musoma Mjini kumpa ushirikiano kwa kuhakikisha vikundi vinaanzishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles