31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

DC Njombe awatahadharisha watakaouza taulo za kike za wanafunzi

Na Mwandishi wetu,Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri ameonya na kuwatahadharisha wasimamizi wa wanafunzi watakaothubutu kuchepusha na kuingiza sokoni taulo za kike zilizokabidhiwa kwa shule 28 za sekondari mjini Njombe kwa ajili ya matumizi ya wasichana waliopevuka.

Msafiri ametoa onyo hilo leo Januari 7, wakati akikabidhi vifaa hivyo vilivyonunuliwa na halmashauri ya Mji Njombe kwa ajili ya wanafunzi ili kuwasaidia kuongeza muda wa kuhudhuria vipindi darasani pamoja na kuongeza ufanisi katika elimu kwa wasichana.

“Sio mtoto anapewa taulo siku mbili harafu hazionekani tena, na kuna wengine wakipewa hizi zinaingia kwenye biashara,hilo ni kosa kubwa,” amesema Msafiri.

Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe, Iluminatha Mwenda, amesema wamefanikiwa kununua vifaa hivyo boksi 260 za taulo za kike zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni tisa kupitia mapato yao ya ndani na kukabidhi shule 24 kwa ajili ya wasichana 5636 waliopevuka ili kuwasitiri wanapokuwa hedhi.

“Tumenunua taulo za kike kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri kwa wasichana ya kusoma vizuri, na katika bajeti yetu tumetenge Sh milioni 10 kwa ajili ya sekondari na milioni 10 kwa ajili ya shule za msingi. Leo tumewakabidhi sekondari,”amesema Iluminatha.

Valeno Kitalika ni Mkuu wa shule ya sekondari Joseph Mbeyela, kwa niaba ya wakuu wa shule wameishukuru serikali kwa msaada huo kwa ajili ya watoto kwa kuwa wataongeza ari ya kujisomea huku akitoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitolea.

“Nimshukuru mkurugenzi na serikali ambao wameweza kutoa vifaa hivi kwa watoto,hawa watoto sasa wataongeza ari ya kusoma kwasababu ni vitu ambavyo vilikuwa vinawakwamisha kutokana na mahudhurio kuwa hafifu,”amesema Kitalika

Akizungumza mara baada ya kupokea taulo hizo mwanafunzi, Steria Muta kutoka shule ya Sekondari  Maheve ameshukuru serikali kwa msaada huo huku wakiendelea kuwasaidi kwa kuwa shule zingine ziko maeneo ya pembezoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles