25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

DAWASA yaahidi maji Kibaha vijijini

Na Gustafu Haule,Pwani

Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA), Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya ziara ya kukagua Mtambo wa maji uliopo eneo la Mlandizi katika Halmashauri ya Kibaha vijijini na kuahidi kuwa mpaka ifikapo Desemba mwaka huu changamoto ya maji itakuwa imekwisha.

Ziara ya Mkurugenzi huyo imetokana na maombi ya Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini, Michael Mwakamo(CCM) baada ya kuona bado katika Jimbo lake linachangamoto ya ukosefu wa maji.

Kwa mujibu wa mbunge huyo amesema kuwa Mlandizi kuna mtambo mkubwa wa maji lakini chakushangaza bado yapo maeneo ambayo wananchi wake wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maji.

Akiwa katika ziara hiyo Mbunge Mwakamo amemuomba Mhandisi Luhemeja, kuhakikisha Dawasa inafanya jitihada ili kupeleka maji katika maeneo yenye mahitaji ili kuweza kuokoa maisha ya wananchi wa Kibaha vijijini.

Kufuatia maombi hayo, Mhandisi Luhemeja amemtoa wasiwasi mbunge huyo kwa kusema kuwa Dawasa itahakikisha ifikapo Desemba mwaka huu maeneo yote yatakuwa yamepata maji huku akisema mradi wa Mabwawa umefika asilimia 95 na mradi wa Soga unaendelea vizuri.

Mhandisi Luhemeja amesema Dawasa inafanyakazi ya kuhakikisha wanancho wote wa jimbo hilo wanapata huduma bora ya majisafi na kwamba eneo hilo ni miongoni mwa yale yenye kipaumbele.

“Jimbo la Kibaha Vijijini ni moja ya maeneo ya kipaumbelea mbayo Dawasa imepanga kuyafikishia huduma muhimu ya maji safi na salama ifikapo mwishoni mwa waka huu, kwani kama tunavyofahamu kwamba hapa ndipo kuna mtambo mkubwa halafu wasipate maji hilo haliwezekani.

“Hivyo kufikia Desemba mwaka huu wananchi watapata maji ya uhakika,” amesema Mhandisi Luhemeja.

Naye, Diwani wa Kata ya Kawawa, Alfred Malega, amemshukuru mbunge huyo kwa jitihada za kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya maji jimboni humo huku akisema kwa jitihada hizo Mlandizi itapata maji.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles