Na Mwandishi Wetu, Makete
Mbunge wa Makete, Festo Sanga ameshirikiana na wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mang’oto kufanya kazi ya maendeleo kwa kusafisha Intake ya maji iliyopo kwenye milima umbali wa kilomita 8 kutokea kijiji cha Malembuli.

Akizungumza mara baada ya kukamilikia kwa zoezi hilo la usafi, Sanga amesema kuwa wametumia zaidi ya masaa mawili kutekeleza hatua hiyo muhimu katioka kuhakikisha kuwa wannachi wa Mang’oto wanapata maji.
“Mimi pamoja na wananchi wangu tumetumia karibu masaa mawili katika kuhakikisha kuwa tunapanda mlima huo na baadae kufika eneo lililotegwa maji ambalo takribani wiki nzima limeziba na kusababisha ukosekanifu wa maji kwa wananchi wa Mang’oto.
“Nawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, furaha yangu ni kujumuika nanyi kwenye kazi hii ambayo kwa leo imeleta matumaini ya kupatikana kwa maji, nawashukuru kwa uchaguzi, mmetuamini tushirikiane kwenye kuchapa kazi,” amesema Sanga.
Mbali na kushughulikia changamoto hiyo ya maji, Sanga pia amefanikiwa kutimiza ahadi yake ya kuwezesha huduma ya umeme kwenye Zahanati ya Ilindiwe ambayo amefunga Sola kwa ajili ya kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa saa 24.