Na PATRICIA KIMELEMETA
MBUNGE wa Viti Maalumu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Upendo Peneza, ambaye naye amekuwa akitajwa kuwa na mpango wa kukihama chama hicho, ameibuka na kukanusha taarifa hizo, zaidi akieleza kutopendezwa na hatua ya wabunge wanaohama vyama vyao, kwani wanaliingiza Taifa kwenye hasara kurudi kwenye uchaguzi kabla ya muda wake.
Kauli ya Peneza imekuja siku moja baada ya Mbunge wa Jimbo la Siha (Chadema), Dk. Godwin Mollel, kutangaza kukihama chama hicho na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Peneza, mbali na kueleza hasara ambayo wabunge hao wanalitia Taifa, alihoji mantiki ya sababu wanazozitoa wabunge hao hadi kufikia hatua hiyo ngumu.
“Nimeshangazwa sana na baadhi ya wabunge wanaohama vyama kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli, wakati waliweza kufanya hivyo hata wakiwa kwenye vyama vyao, hiyo siyo hoja na wala haina mantiki,” alisema Peneza.
Peneza, ambaye pia alieleza japo si kwa undani changamoto anazozikabali ndani ya chama chake, lakini alisisitiza umuhimu wa kuheshimu kodi zinazotolewa na Watanzania kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya Taifa lao.
“Tunakwenda kwenye uchaguzi, wabunge hawa waliojitoa wakiwa hai, hawajafukuzwa na vyama vyao wameondoka wenyewe, Taifa zima tunaingizwa katika…”
Kwa habari zaidi usikose kununua nakala yako ya Mtanzania leo.