24.7 C
Dar es Salaam
Saturday, April 13, 2024

Contact us: [email protected]

MATIBABU YA LISSU YAMUIBUA NDUGAI

ABRAHAM GWANDU NA SARAH MOSES – DODOMA/ARUSHA

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai, ameibuka na kusema yamesemwa mambo mengi kuhusu Bunge kushughulikia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu, anayetibiwa nchini Kenya,  lakini anaomba waelewe kuwa, kujibishana na mgonjwa aliyepo kitandani haipendezi, ndiyo maana yupo kimya.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, alisema mara kadhaa alishatoa ushauri wa kimya kimya kwa familia ya Lissu kuwa mambo ya Serikali na Bunge huwa yanakwenda kwa makaratasi na hayaendi kwa kuzungumza na vyombo vya habari na kuishia hapo.

“Familia ya Lissu ilitakiwa kuandika barua kama ambavyo taratibu zilivyo, wanaambiwa lakini hawakitekelezi, wakiandika wangepata majibu kwa njia ya maandishi,” alisema.

Kuhusu utaratibu uliotumika kumpeleka Lissu katika Hospitali ya Nairobi anakopatiwa matibabu baada ya Septemba 7, mwaka huu kupigwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana mjini Dodoma, Ndugai alisema hawaulaumu, lakini kidogo ulienda kushoto, tofauti na ule wa kawaida wa Serikali au Bunge.

“Inatakiwa tufanye utaratibu mwingine upya, warudishe jambo hilo katika utaratibu wa kawaida ambao tunaendelea kuwasiliana nao, naamini ipo siku watasikilizana na kusema kuwa jambo hilo si la kuamua yeye kama yeye,” alisema na kuongeza:

“Jambo hili halitatuliki kwa kulaumu katika vyombo vya habari wala kwa kufanya vinginevyo, iwe ni kwa kiongozi wa upinzani hapa bungeni ambaye mara nyingi analaumu kupitia vyombo vya habari.

“Kiongozi wa upinzani yeye bungeni ni namba tatu, kuna spika wa kwanza, wa pili naibu spika, sasa kwanini yeye anashindwa kupeleka dokezo panapohitajika wakati anao uwezo na anayo ofisi pamoja na watumishi pale bungeni.

“Mara nyingi hatupendi kujibu kwasababu ni vitu ambavyo vipo ndani ya ofisi, kwanini rahisi kulaumu akiwa mbali wakati na yeye anayo ofisi bungeni.”

Akizungumzia sababu ya kutokwenda Nairobi kumtembelea Lissu, alisema kama spika, hawezi kwenda kama wanavyokwenda wabunge wengine, kwa kuwa anapokwenda lazima kuwapo na taarifa rasmi za Serikali za kibunge na kupokelewa rasmi.

“Kipindi Lissu amepelekwa Nairobi kulikuwa na sintofahamu ya uchaguzi wa Kenya, hivyo mimi kama kiongozi nilijiongeza kwa sababu kwa wakati ule watu wa Kenya wangedhani labda ajenda niliyoenda nayo ni nyingine na si kumuona Lissu,” alisema.

Alisema kwa kuwa uchaguzi wa Kenya umekwisha, muda si mrefu atakwenda kumtembelea Lissu, baada ya sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya kupita.

Pia alisema aliwatuma wabunge wawili kwa niaba ya Bunge kwenda Nairobi kumtembelea Lissu.

Alisema Oktoba mwishoni aliwatuma wabunge Marry Chatanda kutoka Bara na Faharia Shomari kutoka Zanzibar.

Alisema wabunge aliowatuma ni wajumbe wa Kamisheni ya Bunge au Tume ya Huduma za Bunge na walimtembelea na kumpa salamu za Bunge.

“Tume ya Utumishi wa Bunge ndiyo inayoshughulikia masuala yote yanayohusu maslahi ya wabunge…”

Kwa habari zaidi, nunua nakala yako ya Mtanzania leo

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles