25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

HARUFU YA RAIS KUONGEZEWA MUDA YANUKIA

Na MWANDISHI WETU

HOJA iliyowahi kuibuliwa na Mbunge wa Chemba (CCM), Juma Nkamia na kutaka kuifikisha  ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mabadiliko ya Katiba ya kuongeza muda wa Rais kukaa madarakani kutoka mitano hadi saba, sasa imeibuka upya ndani ya Baraza Wawakilishi mjini Zanzibar, ambako baadhi ya wajumbe wameshauri jambo hilo hilo.

Tayari Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, ameonekana kuuunga mkono ushauri huo, akisema kuwa, ni mzuri na ni suala ambalo linazungumzika bila matatizo.

Balozi Idd aliyasema hayo jana, wakati akifunga mkutano wa nane wa Baraza la Tisa la Wawakilishi, lililoketi kwa takribani wiki moja kujadili mambo mbalimbali.

Itakumbukwa Nkamia aliwasilisha kusudio hilo Ofisi za Bunge mjini Dodoma kwa mujibu wa kanuni ya 81(2) ya kanuni za Bunge toleo la 2016.

Kupitia barua aliyoisaini Septemba 12, akielezea kusudio hilo la kuwasilisha Hoja Binafsi ya Sheria ya Mabadiliko ya 15 ya Katiba.

Hata hivyo, kusudio hilo lilipingwa na watu mbalimbali, wakiwamo wasomi, kama Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Benson Bana na Mchambuzi wa masuala la siasa, Profesa Mwesiga Baregu, ambao walitoa hoja kuwa, linamwongezea Rais muda wa kukaa madarakani.

Oktoba mwaka huu, kupitia ujumbe mfupi aliouandika katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp, Nkamia alisema aliamua kuondoa kusudio hilo baada ya majadiliano na maelekezo kutoka kwa viongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kuibuliwa sasa kwa hoja hiyo ndani ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wakati baadhi ya wajumbe wakichangia Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Tume ya Uchaguzi ya mwaka 1984 na kuweka sheria ya mwaka 2017, huenda nako kukazua mjadala mwingine mpya.

Katika kuchangia huko, baadhi ya wajumbe walisema ili Zanzibar iepuke matumizi, hasa kipindi cha uchaguzi, haina budi kuongezwa kwa muda wa utumishi wa urais.

Akichangia, Mwakilishi kutoka Jimbo la Shaurimoyo, Hamza Hassan Juma, alisema muda wa urais unapaswa kuongezwa, ili kumpa Rais wakati mzuri wa kutumikia wananchi, sambamba na kutekeleza mipango ya maendeleo.

Juma alisema muda wa miaka mitano wa uongozi wa Rais kuwa madarakani ni mdogo na kwamba fedha nyingi za wananchi zinapotea kwa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.

Alisema Uchaguzi Mkuu hutumia fedha nyingi za walipakodi, kiwango ambacho kinaweza hata kujenga zaidi ya shule kubwa 20, ambazo zingesaidia jamii katika kuondokana na uhaba wa shule.

Juma alisema pamoja na Katiba zote mbili (ya Tanzania Bara na Zanzibar) kuweka muda huo wa miaka mitano…

Kwa habari kamili nunua nakala yako ya Mtanzania

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles