24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MKE WA MTU AKANA KUZAA NA NABII MWINGIRA

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MKE wa Dk. William Morris, Dk. Philis Nyimbi, anayedaiwa kuzaa na Nabii Josephat Mwingira, amekana mahakamani kwamba haujui mwili wa nabii huyo wala hajawahi kuzaa naye.

Anadai aliamua mwenyewe kuzaa mtoto na mfanyabiashara ambaye sasa ni marehemu na kwamba mtoto huyo si wa Nabii Mwingira wala Dk. Morris.

Dk. Nyimbi alitoa utetezi huo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini, kwa kuongozwa na Wakili wake, Peter Swai.

Alidai mwaka 2001 alifunga ndoa na Dk. Morris katika Kanisa la Mtakatifu Albano na walikaa mapumziko ya siku tatu katika Hoteli ya Starlight kisha wakahamia Muhimbili alikoishi katika chumba kimoja akiwa kwenye mafunzo ya vitendo.

“Niliishi naye katika chumba kimoja kwa miezi mitatu, aliniahidi tutaenda kuishi Marekani lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda hakukuwa na safari, mwishowe nikaanza kuona aibu kwa madaktari wenzangu, kila wakikaa walikuwa wananiuliza naondoka lini.

“Nilipoona hatuondoki nikaona nimuulize safari yake ina tatizo gani akanieleza kuna tatizo la tiketi, nikamsaidia kumaliza tatizo hilo akafanikiwa kuondoka peke yake Februari, 2002, mimi nikabakia akasema nitamfuata tukaishi huko.

“Mawasiliano yalikuwa ya shida, nilichanganyikiwa sana, madaktari wenzangu walikuwa wakinihoji naondoka lini, nilikuwa nalia tu.

 

Kwa habari kamili nunua nakala yako ya Mtanzania.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles