23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Chadema aiomba Serikali kuwapandisha madaraja Askari Polisi

Na Mwandishi wetu, Dodoma

Mbunge Viti Maalum (Chadema), Agnesta Lumbert, ameiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kuwapandisha madaraja Askari Polisi wanaotakiwa kupandishwa.

Aidha, amesema kuna baadhi ya askari polisi ambao ni wakaguzi wasaidizi tangu mwaka 2015 hawajapandishwa daraja na kuwa wasaidizi kamili hadi mwaka huu jambo ambalo amesema siyo sawa.

Akiliza swali bungeni Februari 11, bungeni mbunge huyo alihoji serikali ina mpango gani wa kuwapandisha madaraja askari polisi hao na kiongeza kuwa Waziri husika (George Simbachawene) anazo taarifa za askari hao.

Akijibu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Khamis, alisema  kuwa hakuna askari polisi ambaye hakupandishwa daraja tangu 2015, na serikali haina taarifa za kama kuna askari ambaye hakupandishwa daraja.

 â€œUnajua jeshi la polisi ni taasisi nyeti hivyo serikali imekuwa ikiwapandisha vyeo pale inapobidi kulingana na bajeti, hivyo hilo suala kutopandishwa madaraja sina taarifa nalo,’’ amejibu Naibu Waziri huyo.

Naibu huyo amesema kuanzia mwaka 2015 hadi 2018 serikali ilipandisha madaraja askari polisi 3,454 wakiwemo wakaguzi wasaidizi 1,163 ambao walipanda vyeo.

Hata hivyo, Khamis amesema serikali itaendelea kupandisha vyeo askari hao kulingana na bajeti itakavyoruhusu.

Aidha, Khamis amesema serikali inawajali askari Polisi kwa kutambua mchango wao mkubwa hapa nchini katika suala la ulinzi na usalama wa raia na mali zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles