29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

GSM HOME yaja na GSM HOME GULIO EXTRA 2021

Na Beatrice Kaiza, Dar es Salaam

Kampuni ya uuzaaji wa Samani za Nyumbani na Ofisini ya GSM Home, imezindua kampeni ya Punguzo la bei la bidhaa zake zote inayofahamika kama ‘GSM HOME GULIO EXTRA 2021’ ili kutoa nfasi kwa wateja na wadau wake kufanya manunuzi katika kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Februari 12, katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika rasmi eneo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Masoko na Mawasiliano GSM, Smart Deus, amesema lengo la kuweka punguzo hilo kubwa ni kuwafikia Watanzania wengi ili waweze kujipatia mahitaji mbalibali kwa bei nafuu.

“Mwaka 2021 utakuwa wenye neema kwa kuleta bidhaa nyingi zenye ubora, bei nafuu na uhakika kwa watumaiji, hivyo baada ya kuhitimisha kampeni yetu ya kufunga mwaka, sasa tunakuja na Gulio Extra ambapo wateja wetu watajizolea vitu mbalimbali kwa bei nafuu sana.

“Kampeni hii itadumu ndani ya mwezi mmoja ambapo inaanza leo Ijumaa Februari 12 hadi 28, kwenye maduka yetu yote manne ya GSM HOME yaliyopo Mikocheni, Dodoma Capital City Mall, GSM Pugu na Mlimani City,” amesema Deus.

Aidha, Deus ameongeza kuwa; “Katika Kampeni hii kila Mtanzania ana fursa ya kushiriki kwa kufanya manunuzi kupitia punguzo kubwa linaloendelea.

“Lengo letu ni kuhakikisha kuwa tunaendelea kuwa wauzaji na watoaji wa huduma bora ili kukidhi mahitaji na kuboresha maisha ya Watanzania kwa bei na nafuu na ubora wa hali ya juu,” amesema Deus.

Ameongeza kuwa, kampuni ya GSM kupitia GSM Home bado inaendelea kufanya uwekezaji mkubwa hapa nchini na inahakikisha kuna vifaa kwa ajili ya kila matumizi ya ndani ikiwemo samani pamoja na vyombo vya jikoni. Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Idara ya MasokoGSM Group of [email protected] .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles