26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Jane Doka: Mwimbaji wa Uingereza anayewazimia Mercy Masika, Christina Shusho

London, England

WIMBI la wasanii kutoka Afrika wanaofanya sanaa zao Ughaibuni limeendelea kuongezeka huku mashabiki wakishuhudia wanamuziki wapya wakiibuka kwenye kila aina ya muziki.

Kutana na Jane Doka, wanamuziki mahiri wa Injili mwenye makazi yake Uingereza ambaye kwa sasa anatamba na wimbo, Unchanging God.

Swali: Jane Doka ni nani na uliingia vipi kwenye tasnia ya muziki?

Jane Doka: Mimi nimeokoka ni mfuasi wa Kristo,mwimbaji na mwandishi wa nyimbo niliyezaliwa nchini Zimbabwe na sasa naishi hapa Uingereza (United Kingdom).

Niliingia kwenye tasnia ya muziki kama msanii wa binafsi mwaka 2009, yangu nikiwa mdogo nilikuwa naimba kwenye vikundi vya injili na timu za kusifu na kuabudu (Praise and Worship Team).

Nilikutana na mtayarishaji ambaye aligundua uwezo wangu na alinialika kurekodi albamu yangu ya kwanza iitwayo ‘Nditumeyi’ (Nitume) na niliitoa 2009 ambapo nilikuwa njia yangu nzuri ya kuitikia wito wangu kwa Mungu.

Swali: Changamoto zipi unakutana nazo unapofanya muziki wako nje ya Afrika?

Jane Doka: Ilikuwa ngumu mwanzoni kupata nafasi huku kwenye ardhi ya kigeni kwa sababu ya tofauti za kitamaduni, lugha, kuelewa jinsi mfumo wao unavyofanya kazi, ukosefu wa fedha, nadhani hizo ndio zilikuwa changamoto zangu kubwa.

Hata hivyo kwa neema ya Mungu, nadhani sasa nimefika mahali ambapo ninaelewa jinsi ya kusimama katika mazingira haya ingawa bado, lazima nitumie hekima nyingi na nguvu kufanikisha yote hayo.

Swali: Unatamani kufanya kazi na waimbaji gani kutoka Afrika Mashariki?

Jane Doka: Natambua kuwa Afrika Mashariki imejaa talanta za kushangaza, kuna wengi ambao ningependa kushirikiana nao. Mwimbaji kama Mercy Masika kutoka Kenya na kutoka Tanzania, ningependa kufanya kazi na Christina Shusho, napenda sauti na moyo wake anavyomwimbia Mungu.

Swali: Mpaka sasa umepata mafanikio gani kwenye huduma yako?

Jane Doka: Ni ngumu kupima ‘mafanikio’ katika huduma, kwa sababu mtu unaweza vipi kupima mambo ya Mungu? Ila katika hali ya kibinadamu nimeshinda tuzo na kutambuliwa katika tuzo nyingi kwenye huduma yangu nchini kwangu kama tuzo za Kimataifa za Africa Gospel Music (AGMA), nimeshiriki jukwaa na waimbaji wakubwa wengi kama vile Nathaniel Bassey.

Swali: Unaweza vipi kufanya majukumu yako ukiwa kama mama, mke na mwimbaji?

Jane Doka: Ni kwa neema ya Mungu tu nakuambia! Daima nasema nina P tatu (prayer, planning and participation of my family) yaani
sala, upangaji na ushiriki wa familia yangu katika yote ninayofanya.
Sijawahi kufanya yote juu yangu, muziki ni kitu ‘chetu’ sio changu peke yangu, inafanya iwe rahisi zaidi. Pia mume wangu anaunga mkono sana huduma yangu. Yeye ndiye mfadhili mkuu na mchungaji wangu binafsi ambaye ninawajibika kwake hiyo inakuwa rahisi.

Swali: Mbali na muziki unafanya shughuli gani nyingine?

Jane Doka: Mimi ni mwanamke mfanyabiashara pamoja na mume wangu na pia hivi sasa ninasoma PhD ya International Education and Development pia ninatumika katika kanisa langu kama mchungaji msaidizi ninayesimamia idara za vijana na muziki pia ninafundisha neno la Mungu.

Swali: Unadhani kizazi kipya cha muziki wa Injili kina shida yoyote?

Jane Doka: Sidhani kama waimbaji wa kizazi kipya wana ‘shida’ , ningesema tu labda kwa baadhi yao ni juu ya kuelewa umuhimu wa kukaa na Kristo wakati wa kufanya muziki wa injili, kulinganisha mtindo wa maisha na ujumbe ambao wanaweka kwenye nyimbo zao. Sisi ni nuru ya ulimwengu na hatupaswi kufuata mfano wa ulimwengu huu.

Swali: Kwenye wimbo wake Unchanging God ujumbe gani ulitaka uwafikie watu?

Jane Doka: Kwenye Unchanging God, nilitaka kuwakumbusha watu kwamba ingawa mambo yanaonekana kubadilika ulimwenguni, Yesu Kristo ni yeye yule jana leo na hata milele. Yeye habadiliki na ahadi zake zinabaki vile vile. Mungu ni mtawala na habadilishwi na uzoefu wetu. Hatupaswi kamwe kutilia shaka upendo wake kwetu.

Swali: Tumeanza mwaka 2021, mipango yako ni ipi?

Jane Doka: Mwaka huu nitawaletea watu mradi wangu unaitwa Journey to the Faith Project. Huu ni mradi wa muziki uliobuniwa ili kuhamasisha imani kwa Mungu kwa nyakati hizi ambazo ulimwengu uko.

Nitakuwa nikitoa nyimbo zilizoongozwa na Mungu kwa wakati tunapoendelea na safari hii ya imani hadi hatimaye tutatoa albamu ya Faith Project.

Kuna mchanganyiko wa nyimbo za Kiingereza pia nyimbo katika lugha yangu ya asili ya shona. Nitakuwa nikitoa video za muziki pia na ninapanga maonyesho kadhaa ya moja kwa moja yaani ‘live performance’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles