25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MBUNGE ALAZWA KATIKA TAASISI YA TIBA YA MOYO YA JK

NA VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM


pg-3MBUNGE wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), amelazwa katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) akipatiwa matibabu baada ya kupata tatizo la  shinikizo la damu.

Zungu alifikishwa hospitalini hapo juzi jioni akitokea  Hospitali ya Amana ambako alipatiwa matibabu ya awali.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Zungu alisema anamshukuru Mungu sasa hali yake inaendelea vizuri.

“Hali yangu ilikuwa mbaya, nilianza kujisikia vibaya saa 8:30 mchana juzi nikiwa nyumbani, ikabidi wanipeleke  Amana. Walininipatia huduma na saa 12.00 walinihamishia  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

“Nilipokelewa pale ‘emergence’, baadaye nikahamishiwa  JKCI.  Waliponipima waligundua ‘pressure’ yangu ipo juu… kazi zetu zina msongo wa mawazo mengi ndiyo maana ilipanda ghafla,” alisema.

Aliwashukuru madaktari wote waliomhudumia na kuwakumbusha watanzania kupima afya zao mara kwa mara.

“Nawahimiza pia kukata bima ya afya maana ndiyo iliyoweza kunisaidia kupata huduma bora na wao waone umuhimu huo,” alisisitiza.

Mkurugenzi wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema bado wanaendelea kuchunguza afya ya mbunge huyo kujua tatizo gani hasa lililosababisha  shinikizo  la damu kuwa juu.

“Taasisi yetu inatibu watu wanaougua magonjwa ya moyo, siwezi kusema moja kwa moja iwapo Zungu ana tatizo la moyo, tunachunguza kujua sababu za shinikizo lake kupanda,” alisema.

Alisema wana imani kwamba hadi kufikia wiki ijayo watamruhusu kurejea nyumbani kuendelea na shughuli zake za kila siku.

“Nasema hivi kwa sababu hali aliyokuja nayo ni tofauti na alivyo sasa, hadi nyie (waandishi) ameweza kuzungumza  nanyi.

“Jambo ambalo Watanzania wanapaswa kutambua mtu yeyote aliyeanzishiwa dozi ya matatizo haya ya ‘pressure’ anapaswa kuzitumia katika kipindi chote cha maisha yake hapa duniani.

“Tunapata wagonjwa wengi ambao tuliwagundua kuwa na tatizo hili walipoanza dawa na kuona wanaendelea vizuri wakaacha leo hii wanarudi wakiwa wagonjwa zaidi, wakumbuke kuacha kutumia dawa ni makosa makubwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles