26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge alalamikia mfumo wa elimu nchini

chadema_financeNA SAFINA SARWATT, MOSHI

MBUNGE wa Moshi Vijijini, Anthony Komu (Chadema), amesema Watanzania wengi ni masikini kwa kuwa mfumo wa elimu uliopo nchini ni mbovu.

Komu aliyasema hayo juzi katika Tarafa ya Kibosho Magharibi alipokuwa kwenye ziara na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga.

Wakati wa ziara hiyo, Komu alilenga kusikiliza kero za wananchi na kukutana na viongozi waliomaliza muda wao wakiwamo wenyeviti wa vijiji na madiwani.

“Watanzania wanatakiwa kujengewa misingi bora ya elimu ili waondokane na dhana ya kutegemea ufadhili katika kuwaletea miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Kwa miaka mingi, Watanzania hawajengewa misingi bora ya kujitegemea kupitia elimu wanayoipata na jambo hili linasababisha wengi wao kuwa masikini na tegemezi.

“Ili kukabiliana na matatizo haya, ni vema sasa sisi viongozi tukawa mfano bora na kuwajengea uwezo tunaowaongoza.

“Kimsingi, Tanzania hakuna haja ya kuomba ufadhili kutoka nje ya nchi kwa sababu tuna utajiri wa rasilimali nyingi.

“Kwa hiyo kama sisi viongozi tutaachana na porojo za kisiasa na kuungana kwa pamoja kwa kujadili namna ya kuboresha nchi yetu na maisha bora ya wananchi, hakuna haja ya kuwaomba wafadhili waje kutufadhili,” alisema Komu.

Akizungumzia muda wake wa uongozi, alisema atashirikiana na viongozi wa ngazi za vijiji na kata ili iwe rahisi kwake kutatua kero sugu za wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles