28.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

CCM Mufindi wajiandaa kufukuzana

DSC_0926NA GUSTAPHU HAULE, IRINGA

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa, kinaendelea kufanya uchunguzi dhidi ya wanachama waliofanya usaliti wakati wa uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Baada ya uchunguzi huo kukamilika, wasaliti wote watatimuliwa ili kubaki na wanachama wenye nia njema na chama hicho.

Taarifa hiyo ilitolewa jana na Katibu wa CCM Wilaya ya Mufindi, Jimson Mhagama, alipokuwa akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake kuhusu mwenendo wa chama wilayani hapa.

“Katika hali ya kuendelea kuimarisha chama, kwa sasa kuna utaratibu wa vikao unafanyika ndani ya wilaya kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa kubaini wanachama ambao ni wasaliti.

“Wasaliti wanaotafutwa ni wale waliosababisha kupungua kwa idadi za kura za wagombea, waliohusika na upotevu wa kata na waliohusika kutoa taarifa za ndani ya chama na kuzipeleka kwa wapinzani.

“Baada ya wasaliti hao kubainika, uamuzi sahihi utatolewa katika vikao halali vya chama na kisha hatua za kutoa adhabu zitafuata ikiwa ni pamoja na kuwanyang’anya kadi wasaliti hao.

“Lengo la kufanya hivyo ni kuendelea kukilinda Chama Cha Mapinduzi kwani ni bora tukabaki na wanachama wachache walio makini kuliko kubaki na wanachama wengi wasiokuwa na faida katika chama,” alisema Mhagama.

Pamoja na hayo, aliwataka viongozi wa CCM wilayani hapa kuhakikisha wanashirikiana na Serikali ili kuleta maendeleo ya haraka.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles