30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Chambo ataja thamani ya Tanzanite iliyokamatwa

Omar-ChamboTERESIA MHAGAMA NA ASTERIA MUHOZYA

KATIBU Mkuu, Wizara ya Nishati na Madini, Omar Chambo, amesema Tanzanite iliyokamatwa wakati ikitoroshwa kwenda nje ya nchi Desemba 15 mwaka huu kupitia Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA), imefikia thamani ya Dola za Marekani milioni 1.2

Chambo aliyasema hayo jijini Arusha jana wakati wa kikao chake na Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara, zinazodhibiti utoroshaji wa madini kwa pamoja.

“Tanzanite hiyo ghafi yenye uzito wa gramu 2,015.59 ilikuwa ikitoroshwa na raia wa India, Jain Anurag, aliyekuwa akitaka kuelekea mji wa Jaipur kwa kutumia ndege ya Shirika la Ndege la Qatar.

“Katika hili, nataka niwaeleze Watanzania wanaoshirikiana na raia wa kigeni kutorosha Tanzanite, kuwa wajiepushe na biashara hii haramu  kwani hatua kali zitaendelea kuchukuliwa dhidi yao.

“Baada ya tukio hilo, madini hayo  yaliyokamatwa yameshataifishwa kama ambavyo sheria na kanuni za madini zinavyoelekeza na zoezi hilo la ukamataji hufanywa na Wizara ya Nishati na Madini kupitia Wakala wa Ukaguzi wa Madini (TMAA) kwa kushirikiana na taasisi nyingine kama Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Idara ya Uhamiaji.

“Pamoja na hayo, Serikali itafuta leseni za wafanyabiashara wa madini watakaobainika kutorosha rasilimali hiyo nje ya nchi ikiwemo kuwakamata wachimbaji na wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi stahiki kwa Serikali.

“Ili kudhibiti utoroshaji madini unaofanywa na wafanyabiashara wenye leseni na wasio na leseni, wazawa na wasio wazawa, tumeshajipanga kwa kushirikiana na kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha ili kudhibiti hali hii ili Tanzania ibaki kuwa kinara wa uzalishaji na uuzaji wa madini haya na sio nchi nyingine,” alisema Chambo.

Kuhusu wachimbaji wadogo nchini, alisema Serikali itaendelea kugawa maeneo ya uchimbaji madini kwa wachimbaji hao ikiwa ni pamoja na kutoa ruzuku, uagizaji wa zana kama baruti na utoaji wa mafunzo.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Kamati za Ulinzi na Usalama za mikoa hiyo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Amos Makalla, ametoa saa 24 kwa raia wa kigeni wote wanaojihusisha na biashara ya madini ya Tanzanite na madini mengine kinyume cha sheria, kuondoka nchini kabla hawajachukuliwa hatua.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles