Ramadhan Hassan,Dodoma
Mbunge wa Kaliua,Magdalena Sakaya (CUF) ameiomba Serikali kuipa mamlaka ya kusimamia sheria, Wakala wa Misitu (TFS) ili waweze kusimamia jambo la kukatwa miti hovyo .
Akichangia leo Mei 24 bungeni wakati wa Mjadala wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka 2019-2020,Sakaya amesema spidi ya ukataji miti nchini ni kubwa hivyo akaitaka Serikali kuipa Mamlaka,Wakala wa Misitu ili waweze kusimamia sheria.
“Ukiangalia Spidi ya kukata mkaa inadhihiridha kwamba hali ya misitu yetu inaenda kuwa hatarini, Wakala wa Misitu wapewe Mamlaka, ukipewa Mamlaka unakuwa na uwezo wa kusimamia.
“Miti inabakwa mbao zinazozalishwa hazijakomaa nataka nipate majibu kwanini mbao ambayo haijakomaa inaingizwa Sokoni.Nini mkakati wa Seriikali,”amehoji Sakaya.
Aidha,Sakaya ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuliongezea bajeti Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa)kwani lina majukumu mengi.
“Serikali isipoangalia vivutio vyetu vitapotea Tanapa tunawapa majukumu makubwa wakati bajeti yake tumeipunguza kwa asilimia 18.Serikali ni lazima ikubali ipunguze tozo Tanapa imefanya kazi kubwa sana,kiukweli wanatakiwa kuongezewa bajeti tusipokuwa makini tunaenda kuiua Tanapa,”amesema Sakaya.