21.5 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge abaini madudu zabuni za ujenzi Kibamba

Na Vincent Mpepo, OUT

Mbunge wa Jimbo la Kibamba, Issa Mtemvu ameeelezea kusikitishwa kwake kufuatia utekelezaji mbovu wa zabuni na kadarasi za ujenzi wa miundombinu katika jimbo la Kibamba na kuahidi kufuatilia kwa karibu ili kuwepo na thamani ya pesa inayowekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu hiyo.

Hayo yamebainika jana katika ziara yake kwa wananchi wa jimbo hilo yenye lengo la kuwashukuru kwa kumchagua na kuanisha mipango aliyonayo katika utendajikazi ili kuwafanikisha utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Akiwa katika kata ya Kibamba Mtemvu amesema kumekuwa na ubabaishaji wa utoaji wa kandarasi na zabuni katika ujenzi wa miundombinu hususani madaraja na vivuko ambao umesababisha ujenzi wa miundombinu isiyokidhi viwango.

“Nimeshuhudia madaraja na vivuko ambavyo havipitiki licha ya kuwa ujenzi wake hauna muda mrefu suala linaoonesha kuwa kuna shida”, alisema Mtemvu.

Aidha, amewataka watendaji wa serikali na viongozi wa chama jimboni mwake kutekeleza wajibu wao ili kuitendea haki nafasi walizonazo katika kuhakikisha thamani ya pesa inaendana na ubora wa kazi au miundombinu inayojengwa.

Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Ubungo Pili Mustafa aliwashukuru wanachama wa CCM Kata ya Kibamba hususani akina mama na vijana ambao walijitokeza kwa wingi wakati wa upigaji kura ambao umeleta matunda mazuri ambayo ni ushindi kwa CCM.

“Niwashukuru akina mama, vijana na wote mlioshiriki katika kuichagua CCM kwa kumpigia kura Diwani, Mbunge na Rais”, amesema Pili.

Amesema kazi iliyobaki ni kuwasaidia viongozi katika utekelezaji wa majukumu yao ambayo ni kutoa taarifa za kero zilizopo ili wasaidie katika kupata ufumbuzi na hatimaye maendeleo ya jimbo na taifa kwa ujumla.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ubungo, Lucas Mgonja alimpongeza Mbunge wa Jimbo hilo kwa kukukumbuka kurudi na kuwashukuru wananchi kitu ambacho kinatoa matumaini kwao kwa kiongozi wao yupo na anawakumbuka.

Amesema ni viongozi wachache hukumbuka kuwashukuru wananchi hivyo amemtaka Mbunge huyo kuendelea na utamaduni huo kwa kuwa ni njia ya kupata mrejesho wa kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hivyo kuweza kuwasemea bungeni kwa ushahidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles