30.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Walioharibu fedha BoT kizimbani

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Serikali imewafikisha Mahakamani waliokuwa watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) nane na wenzao watano kwa tuhuma mbalimbali ikiwemo kuharibu noti 460,000 za 10, 000 na kuisabbaishia benki hiyo hasara ya zaidi ya Sh bilioni 4.6.erikali

Washtakiwa hao wamefikishwa leo Jumatatu, Desemba 14, asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Godfrey Isaya. 

Wakisomewa mashtaka na jopo la mawakili wanne wa Serikali likiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Poul Kadushi, aliwataja washtakiwa kuwa ni Mariagoretha Kuzugala, Henry Mbowe, Asha Sekiboko, Cecilia Mpande, Agripina Komba, Zubeda Mjewa, Khadija Kassunsumo na Mwanakheir Omary. 

Washtakiwa wengine ni Alistides Genand, Shukuru Mchegage, Musa Chengula, Zaituni Chihipo na Respicius Ishengoma ambao walisomewa mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya. 

Inadaiwa kuwa kati ya Januari mwaka 2017 hadi Septemba 30 mwaka 2019, watumishi hao wa BOT kwa kuvunja majukumu yao ya kazi waliwezesha utendekaji wa kosa la kuongoza genge la uhalifu. 

Shtaka la pili, inadaiwa kuwa, katika tarehe hizo na maeneo hayo, jijini Dar es Salaam, washitakiwa  Genand, Mchegage, Chengula,  Chihipo na Ishengoma wakiwa si watumishi wa BoT, kwa kushirikiana na watumishi hao wa BoT kwa makisudi, waliwezesha kutendeka kosa uharifu wa kupanga. 

“Shtaka la tatu , inadaiwa kwamba, katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote bila ya kuwa na kibali na kutokuwa wazalendo, washtakiwa wote waliharibu noti kwa kukata noti 460,000 za 10,000 sawa na Sh bilioni 4.6.

” Washtakiwa mnadaiwa kwa ulaghai, kwa kujua na kwa mpango wa kitapeli mlijipatia faida ya Sh bilioni 1.533 kutoka BoT baada ya kuwasilisha noti hizo BoT,”amedai Kadushi.

Washtakiwa wote katika tarehe hizo jijini Dar es Salaam, waliisababishia BoT hasara ya Sh bilioni 4.6.

Wakili Kadushi amedai, upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, washtakiwa wamerudishwa rumande, kesi itatajwa Desemba 28 mwaka huu. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles