25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Mbilikimo washiriki mitindo kubadili mtazamo kuhusu urembo

wakipita-jukwaani

NA JOSEPH HIZA, DAR ES SALAAM

WANAWAKE wafupi warembo wameweza kuvunja mtazamo wa miaka mingi kuwa urembo na au uanamitindo ni kwa warefu, wenye miguu mirefu na wembamba pekee.

Ni kupitia maonesho ya mitindo ya mavazi yanayopigiwa chapuo na taasisi isiyo ya kiserikali ijulikanayo la Onesho la Kimataifa la Mitindo la Mbilikimo.

Taasisi hiyo, inayoitwa Onesho la Taifa la Mitindo la Mbilikimo ilianzishwa mwaka mwaka 2014 mjini New York Marekani baada ya kuona changamoto zinazowakabili mbilikimo.

Tayari imechochea kufanyika kwa mashindano ya mitindo ya mavazi kwa mbilikimo katika miji ya New York, Paris, Berlin na hivi karibuni mjini Tokyo Japan.

Taasisi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwamo serikali hulenga kuinua uelewa na mwamko kuhusu umbilikimo.

Huwashirikisha katika maonesho hayo kufuatia changamoto zinazowakabili kupata mavazi yanayowafiti.

Kubwa zaidi kuliko yote maonesho haya huendesha kampeni za kubadili mtazamo wa jamii kuhusu tasnia nzima ya urembo kwa ujumla wake na vigezo vya aina ya washiriki.

Hivi karibuni mjini Tokyo, Japan wanawake mbilikimo sita waliweza kushiriki onesho la kimataifa la mitindo kwa mbilikimo.

Picha zikionesha warembo hao wakipingana na dhana kuwa urembo ni kwa ajili ya warefu pekee wakiwa wamependeza na mavazi yao wakati wakitembea kwa miondoko ya kipaka huko Ebisu, zilivutia hadhila. Ni onesho la mavazi lililofana mno.

Hivyo, waliweza kuonesha kwamba wanamitindo wanaweza kutokana na maumbo na saizi yoyote ile kuliko inavyofikiriwa sasa.

Kwa kawaida wanamitindo wanafahamika  kuchaguliwa wakiwa na vigezo vya urefu si chini ya mita 1.30.

Na washiriki hawa ‘twiga’ kutoka duniani kote husafirishwa katika madaraja ya juu ya ndege na kuwekwa katika hoteli za kifahari kwa kushiriki maonesho hayo.

Hali kama hizo zinazowafanya wahusudiwe huwafanya wanawake wengine kuhesabiwa hawana sifa na au si warembo.

Kitendo hicho huwaathiri wengine kisaikolojia au hujikuta wakiingia katika mkumbo wa kujitengeneza miili yao kwa kupandikiza plastiki, kitu ambacho kinafahamika ni hatari kwa afya.

Shoo hii ya Japan inafanyika kwa mwaka wa tatu ikiwa tayari imefanyika katika miji ya Paris na New York kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita.

Katika onesho la mwaka jana mjini Paris, ambalo liliandaliwa na Wizara ya Utamaduni ya Ufaransa, ikiwa ni sehemu ya kampeni ya serikali kusaidia kuhamasisha viwango mbadala vya urembo katika tasnia hiyo inayopendelea warefu na wembamba.

Lilifanyika baada ya waandaaji kuishutumu vikali tasnia ya urembo nchini humo kwa kubagua wanawake wengine.

Wanawake mbilikimo 15 wenye urefu wa futi nne walishiriki kwa mavazi tofauti tofauti ya kisasa yaliyobuniwa na wabunifu maarufu mjini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles