24 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Unavyoweza kutumia kamera ya Smartphone kujifunza lugha

androidpit-google-translate-1-w782

Na FARAJA MASINDE,

HIVI ni mara ngapi umenunua dawa halafu ukashindwa kuelewa lugha iliyoko kwenye karatasi ya maelekezo, nje ya maelezo ya daktari?

Au ni mara ngapi umewahi kukosa huduma kutokana na kutoelewa lugha anayotumia mtoa huduma, huku ukiwa umeshikilia Smartphone yako mkononi?

Najua majibu unayo. Usikubali tena kubaki nyuma, kuwa wa kisasa kwa kuifanya simu yako ya Smartphone ikupe faida kwenye maisha yako ya kila siku.

Sasa hivi unao uwezo wa kwenda hata Misri kama si China na ukatumia Smartphone yako kuwasiliana na yeyote licha ya kutokujua Kichina au Kiarabu.

Najua unajua kuwa tunaishi kwenye dunia inayokimbia mno, kila kitu kwasasa kinarahisishwa na teknolojia.

Kama hujui ichukue hii… unaweza kupakua (Download) programu ya Google Translate App itakayokusaidia kujua lugha yoyote kwa haraka zaidi.

Msaada wa App hii unakuja pale ambapo unakutana na maandishi usiyo yafahamu mahala popote iwe ni dawa au hata sehemu yoyote ambayo kupata huduma kunahitaji kujua lugha inayotumiwa na mtoa huduma ambayo ni ngeni kwako.

Hivyo, pindi unapokutana na lugha hiyo usiyoifahamu unachotakiwa kufanya ni kufungua Smartphone yako kisha fungua App yako niliyokueleza hapo juu ambayo imetengenezwa kwa mfumo wa kamera.

Mara baada ya kufanya hivyo, jukumu lako litakuwa ni moja tu kuhakikisha kuwa unategesha kamera yako kwenye maandishi hayo au kutegesha karibu na ipotokea sauti hiyo ambayo ni ngeni kwako ambapo App hiyo itaanza kukueleza kwa lugha unayoitaka wewe.

Ili uweze kutumia App hii ambayo inapatikana kwa watumiaji wa Android na iOS kwa wale wenye iPhone, kazi yako ni kuhakikisha kuwa unakifurushi cha Internet kwenye simu yako.

App hii ina zaidi ya lugha 90 huku ikiwa na maneno zaidi ya milioni 100 ya lugha zote unazozifahamu duniani huku ikifanyiwa maboresho mara kwa mara.

Hivyo, itumie simu yako vizuri ili uweze kupata unachotaka kwani kukua kwa teknolojia kumeifanya simu yako kuwa si tu kifaa cha mawasiliano bali pia kuna mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kukufanya uifurahie zaidi dunia.

Huduma hii inafanyakazi kwa haraka zaidi kuliko unavyofikiri.

0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles