24.2 C
Dar es Salaam
Monday, May 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mbeya City waipa kipa Simba

owen-chaimaNa ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM

UONGOZI wa klabu ya Mbeya City imewaita mezani Simba kuzungumzia usajili wa kipa Owen Chaima, atakayekuwa msaidizi wa kipa Vicent Angban.

Uongozi wa klabu ya Simba umekuwa ukimpigia hesabu huyo wa Mbeya City ili asaidiane na Angban ambaye kwa sasa ndiye tegemeo.

Akizingumza na MTANZANIA Jumapili, Ofisa Habari wa Mbeya City, Dismas Ten alisema kuwa wao wapo tayari kuwaachia Simba kipa huyo iwapo kama wana nia ya kumtumia kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kama watafuata taratibu za kumsajili.

“Chaima ana mkataba na Mbeya City ambao haumruhusu kufanya mazungumzo na timu nyingine, hivyo kama taarifa zinazozungumzwa juu ya Simba kumtaka kipa wetu waje tu mezani tuzungumze.

“Sisi hatuna tabia ya kuwazuia wachezaji wanaotakiwa na timu nyingine, hivyo waje tukae mezani tuzungumze tukikubaliana tunawapa bila tatizo kwa kuwa sisi tuna wachezaji wengi wenye uwezo, hivyo tukimruhusu Chaima haina maana tutapoteza kitu kikubwa ila itatoa nafasi kwa wengine,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles