Arodia Peter, Dodoma
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), Â amewashauri wabunge kuondoa tofauti zao na kuhakikisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatengewa fedha za kutosha ili kuokoa elimu ya Tanzania.
Mbatia ametoa ushauri huo wakati wa mjadala wa wizara hiyo bungeni leo Aprili 30, ambapo amesema sekta ya elimu inahitaji utulivu na kukubaliana kama taifa mustakabali wa kizazi hiki na kijacho.
“ Lazima  tuwaze kwa upana namna gani tunakuza watoto wetu, namna gani tunawapa uwezo walimu wetu ambao ni walezi wakuu wa taifa letu waweze kuliangalia taifa na kuwa watulivu.
“ Sasa hapa kila siku tunapiga kelele, Naibu Waziri, Ole Nasha chonde chonde tuache tofauti zetu, tuwe na utulivu wa ndani, tuondoe tofauti zetu kutubaliane namna ya kulea watoto wetu,” amesema Mbatia.