29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Mbaraka Mwishehe alimrudisha Mzeru kwenye muziki

mbaraka

NA VALERY KIYUNGU

JUMAMOSI tulivu tunakutana hapa kwenye safu hii ya Old Skuli. Hapa ndiyo mahala ambapo mashabiki na wadau wa burudani tunapata wasaa wa kufahamu mambo kadha wa kadha yanayohusu muziki wa zamani na wasanii wake.

Safu hii imekuwa ikikukutanisha na wanamuziki mbalimbali na kukupa nafasi ya kuwafahamu, leo pia Old Skuli inakukutanisha na Maurus Mzeru ambaye aliwahi kuwika kwenye tasnia hiyo ya muziki miaka mingi iliyopita.

HISTORIA YAKE YA MUZIKI

Ndani ya muziki alianza kufanya kazi zake mwaka 1969 pale alipojiunga na bendi ya Afro 70 iliyokuwa inaongozwa na mwanamuziki mahiri ambaye hivi sasa ni marehemu, Patrick Balisidya.

Mkongwe huyo ambaye hivi sasa amejiwekea makazi yake Tandika jijini Dar es salaam akiendelea na kazi zake za muziki.

Hakudumu sana kwenye bendi ya Afro 70 akaamua kuhamia kwenye bendi ya Kurugenzi Jazz iliyokuwa na makazi yake mkoani Arusha.

Mwaka 1994 Mzeru alisafiri kutoka Dar es Salaam hadi mkoani Tanga,  ambako alikwenda kuanzisha na kuwa mwasisi wa bendi ya Bandari –Tanga ambako hakukaa sana alirejea tena Dar es salaam.

AKUTANA NA MBARAKA MWINSHEHE

Mzeru alikutana na Mbaraka mwaka 1976 kwenye ukumbi wa DDC  Kariakoo Jijini Dar es Salaam, wakati mkongwe huyo alipokuwa na bendi yake ya Super Volcano.

Katika mazungumzo yao ukumbini hapo wawili hao, Mzeru ambaye ni mtunzi, muimbaji pia mpiga solo, alimweleza Mbaraka kuwa kwa wakati huo alikuwa amejiweka pembeni na muziki wa dansi.

Wakati huo Mzeru alikuwa mfanyakazi kwenye kiwanda cha kutengeneza redio na betri za National Panasonic.

Baada ya Mbaraka kupata maelezo hayo alimpa ushauri wa kurejea kwenye muziki kwani muziki ni taaluma na akamsisitiza popote alipo aanzishe bendi ili kuendeleza kipaji alichonacho.

AUNDA NATIONAL PANASONIC SOUND

Kufuatia ushauri huo wa bure kutoka kwa Mbaraka, Mzeru ndipo alipoamua kuunda bendi yake ya National Panasonic hiyo ilikuwa mwaka 1980 baada ya mwajiri wake kumuunga mkono.

Baadhi ya wanamuziki walioshirikiana naye kuunda na kuasisi bendi hiyo ya National Panasonic ni pamoja na Shaka Msuwamwili na Manyama Ladislaus  ambao chini ya uongozi wa Mzeru waliweza kufanya kazi nzuri.

Waliweza kutunga, kurekodi  na kuimba  nyimbo zenye maadili kwa jamii pia zilizoweza kuwagusa wengi, baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na Matatizo ya Ndoa, Kuona ni fahari ya macho ambazo zilikuwa gumzo kwa mashabiki wa muziki wa dansi.

ELIMU YAKE

Alisema shule ya Kati ya Mtakatifu Xavier, ambayo kwa sasa inajullikana kama Kibasila hadi darasa la Nane, akiwa anaendelea kupiga muziki akiwa kwenye bendi ya Gold All Stars, ikiwa inatumiwa na mtindo wa Kalumbende.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles