26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

MBAO YAAPA KUMLIZA TENA PLUIJM

Na MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM

KOCHA Msaidizi wa Mbao FC, Sudi Slim, amesema amebuni mbinu mpya za kumhakikishia ushindi katika mchezo ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Singida United, inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van der Pluijm.

Mbao FC ilianza vizuri msimu mpya wa Ligi Kuu baada ya kuicharaza Kagera Sugar mabao 2-1, huku Singida wakianza vibaya baada ya kukubali kipigo kama hicho kutoka kwa Mwadui FC.

Timu hizo zinatarajia kushuka dimbani Jumatano ijayo kuumana katika pambano litakalopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Singida United itautumia uwanja huo kama uwanja wake wa nyumbani, badala ya ule wa Namfua, ulioko mjini Singida, ambao kwa sasa upo kwenye marekebisho.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Slim alisema anafahamu mchezo huo utakuwa mgumu, kutokana na wapinzani wao kupoteza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Mwadui.

“Mchezo utakuwa mgumu, kwani inafahamika Pluijm hawezi kukubali kupoteza mchezo wa pili mfululizo, hivyo tumeamua kubuni mbinu mpya za kutuhakikishia tunaondoka na pointi muhimu katika mechi hiyo, ili kuendelea kujiweka vizuri.

“Tumepanga kuhakikisha hatupotezi pointi katika mchezo huo, nimezungumza na wachezaji kuhusu umuhimu wa kupata pointi tatu,” alisema Slim, ambaye hakutaka kuweka wazi mikakati yake ya ushindi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles