21.4 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja: Siogopi kutimuliwa Simba

Mayanja-J-1NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, ameweka wazi kuwa yupo tayari kubwaga manyanga kama uongozi wa klabu hiyo hautaridhishwa na mwenendo wa timu na utendaji kazi wake ndani ya kikosi hicho.

Mayanja ambaye amepoteza mchezo mmoja tangu aanze kibarua cha kuinoa timu hiyo Januari mwaka huu, alitamba kuwa tayari amejitengenezea jina kutokana na mafanikio aliyoipa timu hiyo kwa muda mfupi.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema juzi alikutana na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva pamoja na wazee wa Simba ili kujadili namna timu hiyo itakavyoweza kupiga hatua zaidi na kuipa timu hiyo mafanikio makubwa.

“Kwa upande wangu sina tatizo ikiwa uongozi utanitaka niondoke, kwani naamini kwa kazi niliyofanya tayari nimetengeneza jina, Simba si klabu  ya kwanza kufundisha na pia si kazi rahisi timu kufanya vizuri katika msimu wa ligi,” alisema.

Kocha huyo raia wa Uganda, alibainisha kuwa licha ya kuwepo kwa maneno ya watu wasiomtakia mema ndani ya klabu hiyo, atajitahidi kuwajibu kwa kufanya vizuri katika michezo iliyobaki.

“Huu si muda wa kipiga kelele, nitajielekeza kwenye majukumu yangu ipasavyo na si kusikiliza watu wasio na faida na kazi yangu,” alisema Mayanja.

Mayanja aliyeipa Simba ushindi katika mechi 11, alianza kukinoa kikosi hicho baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu Mwingereza, Dylan Kerr, kutokana na kufanya vibaya kwa timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles