26.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja ampa neno Ugando

jackson-mayanja_16c1zw8tqege81g3qbstgngm9zNA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM

KOCHA Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, amesema kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Haji Ugando, anaweza kuwa mchezaji bora zaidi ndani ya kikosi hicho kama ataendelea kufuata masharti ya soka na kujituma uwanjani.

Straika huyo anayekuja kwa kasi katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, alisajiliwa na Simba wakati wa dirisha  dogo la usajili akitokea Jaki Academy ya Mbagala.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mayanja alisema Ugando ni mchezaji mwenye uwezo na amekuwa akionyesha kiwango kilichomvutia akiwa uwanjani, hivyo kama ataendelea kujifunza ataimarika zaidi.

“Mchezaji yeyote mwenye nidhamu na ambaye anafuata maelekezo anayopewa na kocha ni lazima awe na kiwango cha hali ya juu, hivyo kama Ugando ataendelea na kasi aliyonayo atafika mbali zaidi,” alisema.

Katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika juzi Uwanja wa Boko Veteran, jijini Dar es Salaam, kiungo huyo aliwashangaza mashabiki wa Simba kutokana na kiwango alichoonyesha na kufanikiwa kufunga mabao mawili.

Kutokana na umahiri wake uwanjani, mashabiki waliojitokeza kushuhudia mazoezi ya Simba walikuwa wakimmwagia sifa nyingi, huku wakimwelezea kama mchezaji ambaye anaweza kupata mafanikio makubwa ikiwa atalinda kiwango chake.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles