28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tambwe ajipanga kufunika wanaomfuata

tabweNA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga, Amisi Tambwe, amesema atahakikisha anafunga kadri awezavyo kila mchezo, ili kuzima ndoto za wapinzani wake katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tambwe ndiye kinara kwenye Ligi hiyo, kwa kufikisha idadi ya mabao 13, huku mshambuliaji wa timu ya Simba, Hamisi Kiiza, akimfuata kwa karibu baada ya kufikisha mabao 12.

Akizungumza na MTANZANIA, Tambwe alisema kwamba lengo lake ni kunyakua tuzo ya kiatu cha dhahabu msimu huu.

“Michezo haiwezi kuwa sawa, kuna wakati unaweza kufunga na kutofunga, lakini cha msingi ni kuhakikisha kila mchezo naweza kufunga ili kuisaidia timu yangu kupata ushindi, pia kuongeza idadi ya mabao,” alisema Tambwe.

Alisema baada ya kutofunga kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union, ambao alishuhudia timu yake ikifungwa mabao 2-0, mchezo wa leo atahakikisha anafunga bao ili kuendelea kuwa kinara wa ufungaji wa ligi hiyo.

“Hata kama sikufunga siku ya mchezo dhidi ya Coastal Union, bado mimi ni kinara, hivyo sina hofu kwa hilo, najiamini nitafanya vizuri kwenye mchezo ujao,” alisema Tambwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles