28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Mayanja akiri ngoma nzito Simba

mayanjaNA HUSSEIN OMAR, DAR ES SALAAM

KOCHA msaidizi wa Simba Mganda,  Jackson Mayanja, amesema anakabiliwa na shughuli nzito kuhakikisha anaipatia timu hiyo mafanikio katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mayanja aliyekabidhiwa majukumu ya kukinoa kikosi hicho wiki iliyopita baada ya kutimuliwa kwa aliyekuwa kocha mkuu, Dylan Kerr, juzi aliiongoza Simba kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA juzi, Mayanja alikiri kuwa amekuta mapungufu makubwa kwenye kikosi hicho ambacho kinawania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Alisema wachezaji wengi waliosajiliwa kuichezea Simba wamejaliwa vipaji vya soka tofauti na timu nyingine za Ligi Kuu, lakini hawana uwezo wa kuzimudu dakika tisini za mchezo kutokana na kukosa stamina.

Alisema wachezaji wake wana uwezo wa kucheza dakika 45 za kipindi cha kwanza, lakini wanaporudi uwanjani wanachoka haraka na kuwapa wapinzani nafasi za kutengeneza mashambulizi.

“Tumeshinda lakini siwezi kusema kwamba ndio tumemaliza ligi au timu imepata mkombozi kwani bado tuna kazi kubwa mbele ya kufanya kiufundi hasa tatizo la pumzi,” alisema.

Mayanja aliyetimka Coastal Union na kutua Simba, alisema kwa kipindi hiki ambacho amepewa majukumu ya timu hiyo atahakikisha anatumia uwezo wake na kupambana kwa kila hali ili kupata ushindi.

“Ni vigumu kusema nianze kuwapa wachezaji mazoezi ya stamina wakati ligi inaendelea na tayari imeshika kasi,” alisema.

Kwa matokeo ya juzi, Simba imeendelea kubaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imefikisha pointi 30 nyuma ya vinara Yanga wenye pointi 36 sawa na Azam waliopo nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles