JESTINA ZAUYA, TUDARCo
Msanii raia wa DR Congo atayetamba na wimbo wa ‘Songi Songi’, Maud Elka anatarajiwa kutua Jijini Dar es Salaam Oktoba 5, 2021 kwa ajili ya kufanya shoo yake mwenyewe aliyoipa jina la Songi Songi Tour.
Maud amethibitisha kufanya shoo hiyo kupitia ukurasa wake wa Istagram.
Mwanamuziki aliyejizolea mashabiki wengi hapa nchini licha ya kuishi DR Congo, amesema ziara itakuwa ni pamoja na kutembelea vyombo mbalimbali vya habari kuanzia Oktoba 5-12, mwaka huu.
Wimbo wa Songi Songi ni kati ya nyimbo pendwa na inayofanya vizuri hii inatokana na mtindo alioimba.
Ngoma hiyo iliyotoka miezi sita iliyopita imefanyiwa pia remix na msanii mkongwe wa bongo fleva, Ali Kiba aliyoitoa Julai, mwaka huu.