31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, December 2, 2023

Contact us: [email protected]

Yanga tamu, yaweka rekodi ya misimu miwili

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Yanga imeendelea kuwapa raha wadau na mashabiki wake baada ya kuibuka na ushindi katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuifunga Kagera Sugar bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

Aliyepeleka furaha kwa Wanajangwani hao ni kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ dakika ya 24.

Ikumbukwe Wananchi hao walikwenda kuanza ligi hiyo wakiwa wametoka kubeba taji la Ngao ya Jamii wakiwafunga watani zao Simba bao 1-0 kwenye  Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Wanaume kazini

Ushindi huo unaifanya Yanga kuweka rekodi baada ya misimu miwili mfululizo kushindwa kuanza na ushindi.

Msimu uliopita 2020/2021 ilianza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, 2019/2020 ilifungwa nyumbani na Ruvu Shooting bao 1-0.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo uliopigwa leo, Polisi Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KMC, mfungaji akiwa ni Vitalis Mayanga dakika ya 3,20 kwenye Uwanja Black Rhino uliopo Karatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles