27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, May 21, 2024

Contact us: [email protected]

Matusi yamuondoa Jaden Smith kwenye mitandao ya kijamii

BADI MCHOMOLO NA MTANDAO
MTOTO wa nguli wa filamu nchini Marekani, Will Smith ambaye ni mwanamuziki wa hip hop na filamu, Jaden Smith, ameamua kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kupokea ujumbe mbaya kutoka kwa mashabiki wake.
Msanii huyo aliyefikisha jumla ya mashabiki milioni tano katika akaunti yake ya Twitter, amesema sababu hiyo ndiyo iliyomtoa katika mtandao wa Twitter na sasa anajipanga kufunga kurasa zake katika mitandao mingine.
“Siyo lazima niendelee kutumia Twitter, nimeona bora nijitoe kutokana na ujumbe ambao ninaupata kutoka kwa rafiki zangu, hata hivyo, nitajitoa kwenye Facebook kama kutakuwa na hali hiyo.
“Ni bora nibaki kwenye Instagram, japokuwa nimeifunga kwa sasa, pia nitakuwa kwenye mitandao mingine ambayo ninaamini haitakuwa na matatizo kama hayo,” alisema Smith.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles