27.7 C
Dar es Salaam
Monday, February 26, 2024

Contact us: [email protected]

Khadija Kopa: Waimba taarabu wa sasa wamejaa woga na chuki

NA FESTO POLEA
MWIMBAJI wa Taarabu, Khadija Kopa (Malikia Khadija Kopa) ameweka wazi kwamba waimbaji wa taarabu wa siku hizi wanaongozwa na wivu, woga na chuki, ndiyo maana taarabu inaonekana kufa.
Khadija Kopa alisema hayo jana, alipotembelea ofisi za New Habari (2006) Ltd, Sinza Kijiweni, inayochapisha magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania, The African na Rai.
“Wasanii wa taarabu wa sasa wanajenga sana chuki, tofauti na sisi wa zamani tulikuwa tunatengeneza biashara kutokana na ushindani wetu, lakini hawa wa sasa wenyewe kwa wenyewe wanaogopana, hawajiamini na wengine hata kwenye bendi zao wanaogopana,’’ alieleza Kopa.
Kopa aliongeza kwamba taarabu imeshuka kwa kuwa hakuna biashara kama walivyokuwa na marehemu Nasma Hamisi Kidogo, ambapo waliwezesha muziki wa taarabu kuwa juu kuliko miziki mingine nchini.
“Kipindi kile tulikuwa tunatengeneza chuki za biashara wenyewe tupo fresh, lakini tukitangaza onyesho letu watu wanajaa sana, tofauti na sasa wengi wao waoga, wivu, kujisikia na kujenga chuki baina yao wenyewe ndiyo maana taarabu inashuka,’’ alisema Kopa.
Katika hatua nyingine, Kopa alidai kwamba hatima ya kundi lao la TOT bado haijajulikana nani atachaguliwa kuwa kiongozi wa kundi hilo baada ya kifo cha Kapteni John Komba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles