25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Matukio ya unyang’anyi 653 yatokea nchini

Na Debora Sanja, Dodoma

JUMLA ya matukio 653 ya unyang’anyi wa kutumia silaha yametokea katika kipindi cha mwaka 2010 hadi Februari, mwaka huu.
Taarifa hiyo ilitolewa bungeni jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima, wakati akijibu swali la Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi).
Katika swali lake, Mkosamali alitaka kujua idadi ya matukio hayo tangu kipindi hicho, sababu zake na hatua zinazochukuliwa na Serikali.
Silima alisema matukio hayo ya kutumia silaha ni pamoja na utekaji wa magari na uvunjaji.
“Matukio haya yanasababishwa na mwingiliano wa shughuli za kiuchumi na kijamii kutoka nchi jirani.
“Serikali kupitia Jeshi la Polisi imeongeza doria, misako na kuweka vizuizi katika maeneo hatarishi ili kuangalia usalama wa maeneo,” alisema Silima.
Alisema suala la ulinzi na usalama ni wajibu wa kila mwananchi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, jukumu la msingi la Serikali ni kusimamia sheria zinazohusu usalama wa watu na mali zao.
“Natoa wito kwa wananchi wote, hususan waishio mipakani kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii bila hofu, kwani Serikali itahakikisha usalama na amani vinakuwepo na kudumishwa,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles