30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Keissy aitaka Serikali kulipa riba kwa wakulima

ally kessyNa Debora Sanja, Dodoma

MBUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ali Keissy (CCM), ameitaka Serikali kuwalipa wakulima fedha zao pamoja na riba kutokana na kuwacheleweshea malipo yao kwa muda mrefu.
Akiuliza swali bungeni jana, Keissy alisema Serikali imekuwa ikilipa riba mbalimbali kutokana na kuchelewa kulipa madeni ya wazabuni na kutaka wakulima walioiuzia Serikali mahindi yao walipwe riba.
“Serikali inasema nini kuhusu kuwalipa wakulima hao fedha zao pamoja na riba kwa kuwa toka mwaka jana hadi sasa wanadai fedha zao.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Mwijage, alisema Serikali inajitahidi kulipa madeni ya wakulima hao na kwamba kwa sasa inafanya utaratibu wa kutowakopa tena.
Awali akijibu swali la msingi la Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige (CCM), Mwijage alisema uzalishaji na tija ndogo katika zao la pamba umekuwa ukisababishwa na wakulima kupata mapato madogo na hivyo kutokukidhi gharama za uzalishaji.
“Kwa sasa wastani wa uzalishaji wa pamba ni kilo 250 hadi 300 kwa ekari ikilinganishwa na uzalishaji wenye tija wa wastani wa kilo 800-1,000, hivyo kutowezesha wakulima kupata faida hata pale bei ya pamba inapoongezeka,” alisema.
Alisema Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, imeanzisha mashamba darasa katika kila halmashauri inayolima pamba ili kuwafundisha wakulima kanuni za kilimo bora cha pamba.
Alisema pia wizara hiyo kwa kushirikiana na wadau wa zao hilo inaandaa utaratibu wa kuanzisha mfuko maalumu wa kufidia bei za mazao kwa ajili ya kusaidia wakulima pindi bei ya mazao inaposhuka katika soko la dunia.
“Serikali inawahamasisha wakulima wa Mkoa wa Shinyanga kupanda mazao yanayostahimili ukame hususan mtama, muhogo na alizeti kwa lengo la kujikinga na njaa na kuongeza mapato kwa wakulima,” alisema Mwijage.
Katika swali lake, Maige aliitaka Serikali kuweka utangamano wa uzalishaji na bei ya zao la pamba pamoja na kuwahamasisha wakulima wa Shinyanga kulima mazao mengine ya biashara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles