ZAINAB IDDY-DAR ESSALAAM
ZIMEBAKI siku kadhaa kuhitikisha mwaka 2018 na kuingia 2019, huku kila mtu akiwa anatafakari ninialichokifanya katika mwaka unaomalizika.
Ukiachana na maisha ya mtu mmoja mmoja, lakini pia kwenye michezo yapo mengi ya kufurahisha na kusikitisha.
Spotikiki imeona sio vibaya kukumbusha japo kwa ufupi katika miezi 12Â ya mwaka 2018 ni vitu gani vilijitokeza katika soka linalosimamiwa na kuongozwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Fungia fungia/timua timua
Mwaka huu uenda ulikuwa mwaka mbaya kwa baadhi ya wanafamilia wa soka nchini, baada ya kujikutawakipoteza ajira zao  ndani ya TFF aukufungiwa maisha kutojihusisha na soka ndani na nje ya Tanzania.
Inakumbuka miezi michachetangu achaguliwe,Wallace Karia kuwa Rais wa TFF alianza kwa kuwatimua watendajiwa shirikisho hilo ambao walikuwa chini ya Rais aliyemaliza muda wake Jamal Malinzi.
Miongoni mwa waliokutwa na panga hilo ni Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas ambaye alipewa likizo ya lazima hadi mkataba wake ulipokwisha.
Hilo halitoshi, kwani wakati Lucas akipewa likizo ya lazima, Michael Wambura ambaye alikuwa makamu wa Rais, kocha wa Mvuvun wa amekuwa mhanga mkubwa kwa hili, baada ya kufungiwamaisha kutojihusisha na soka, huku kocha wa Mvuvumwa , Joseph Kanakamfumoakipigwa pini ya miaka mitano.
Katika hili yupo pia ClementSanga, mbaye alikuwa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi (TPLB) aliyepita katika uchaguzi mkuu, lakini baada ya miezi mitano kupita, TFF kupitia kamati zake walimuengua kwa madai kuwa aliyestahili nafasi hiyo ni Mwenyekiti wa Yanga , Yusuph Manjina sio makamu wake Sanga.
Rais wa fifa kutembelea nchini
Februari mwaka huu, Tanzania ilipata ugeni mzito katika soka, baada ya kutembelewa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA),Gianni Infatino, ambaye aliongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmed Ahmed.
Ujio wa viongozi hao na viongozi wengine kutoka nchi 19 duniani ulikuwa kwaajili ya kikao cha maendeleo yasoka, ambacho kilifanyika jijini Dar es Salaam Februari22, 2018 ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Ongezeko la usajili kwa wachezaji wageni
Julai mwaka huu, TFF kupitia Kamati yake ya Utendaji ilifanya mabadiliko ya kanuni ya 57, ambapo ilipendekeza ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka saba hadi 10. Kanuni hiyo pia inatoa ruhusa kwa timu za TPL kuwatumia wachezaji saba wa kigeni katika mchezo mmoja.
Kutekwa MO Dewij
Vilio na simanzi vilitawala kwa Wanasimba na familia ya Mohamed Dewij (MO), baada ya kukutwa na tukio la kutekwa na watu wasiojulikana.
MO ambaye ni mwanachama, mmiliki wa klabu ya Simba na mfanya biashara alikutwa na tukio hilo Oktoba 11 mwaka huu, wakati akiingia gym ya Collesium jijini Dar es Salaam.
Mfanyabiashara huyo alikuja kupatikana, baada ya siku tisa tangu kutekwa kwake, akiwa hai huku taarifa zikidai watekaji eneo ya Gymkana.
Simba kutwaa ubingwa baada ya miaka mitano
Baada ya miaka mitano kupita Simba imefanikiwa kuwavua taji la ubingwa watani zao Yanga, baada ya kutawazwa kuwa ndio vinara kwenye LigI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.
Simba ilianza kutangaza ubingwa, baada ya Yanga kupokea kipigo cha 2-0 kutoka kwaTanzania Prisons na kujikuta wakiwa na alama 48, huku Wanamsimbazi wakiwa na michezo mitatu mkononi, ambayo hata kama angepoteza hakukuwa na timu yoyote ya kuwafikia.
Ubingwa wa huo wa ligi umeipa nafasi Simba kupewa kombe, fedha taslimu, lakini pia kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2018/19, mashindano ambayo mara ya mwisho kushiriki ilikuwa msimu wa 2012/13.
Rais Magufuli aipa Stars Mil.50
Oktoba 19 mwaka huu, Rais wa Jamuhuri ya Tanzania, John Pombe Magufuli, aliwakabidhi wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kiasi cha shilingi milioni 50.
Tukio hilo lililovuta hisia chanya kwa wanamichezo, lilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mbele ya viongozi TFF, huku akiwataka wazitumie kwaajili ya mchezo dhidi ya Lesotho ukiwa ni mchezo wa kufuzu AFCON.
Mtibwa mabingwa FA
Juni mwaka huu timu ya Mtibwa Sugar, ilipata nafasi ya kuiwakisha Tanzania katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa 2018/19.
Mtibwa ilipata nafasi hiyo, baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa fainali uliopigwa Juni 2,2018 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha
Kwa mujibu wa sheria na kanuni za TFF, bingwa wa mashindano ya Azam Federation Cup FA ndio atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo Kombe la Shirikisho Barani Afrka.
Ligi bila mdhamini mkuu
Msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulioanza Agosti 20 mwaka huu, umeonekana ni mbaya baada ya kuchezwa bila ya mdhamini mkuu, kutokana na yule wa awali kumaliza mkataba wake na kushindwa kuongeza.
Ligi hii ambayo msimu huu imeshirikisha timu 20, imeonekana kuchezwa kiugumu kiasi cha kukosa fedha za kukidhi mahitaji ya timu, lakini pia kesi za madai kwa wachezaji hivi sasa linaonekana jambo la kawaida katika shirikisho.