Na SWAGGAZ RIPOTA
WAKALI wa Bongo Fleva, Vannesa Mdee, Dayna Nyange, Chege Chigunda, Harmonize, Lady Jay Dee, Aslay, Wolper na wengine wengi wameungana na mastaa weusi kote dunia kupiga biashara ya utumwa inayofanyika nchini, Libya.
Biashara hiyo haramu iliyogundulika mapema wiki hii imefanya mastaa mbalimbali wa burudani kulaani vikali vitendo ya utumwa wanavyofanyiwa waafrika nchini Libya wanaotaka kuingia bara la Ulaya.
Mbali na mastaa hao wa Bongo, wasanii kama Rick Ross, P Didy, Peter wa P Square, T.I, Chris Brown, Omotola Jalade, Tyrese, Bishop Jakes, Davido, Wizkid na Banky W.