25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

NGOMA MPYA ZA DIAMOND, AWAGUSA MA-EX WAKE

Na  CHRISTOHER MSEKENA

HUENDA hana bahati katika sekta ya mapenzi lakini ana bahati ya kupata matukio mabaya na mazuri kwenye mapenzi yanayompa nafasi ya kutengeneza ngoma kali zinazompa mafanikio kimuziki.

Huyu ni Diamond Platnumz ambaye wiki hii amezua gumzo baada ya kuachia nyimbo mbili – Sikomi na Niache zenye uhusiano mkubwa na maisha yake ya mapenzi yaliyopita.

Je, wewe unamtumia / unawatumia vipi kwa faida wapenzi wako wa zamani? Cheki hii ya Diamond Platnumz jinsi anavyowatumia ma-ex wake kujiongezea kipato kupitia muziki wake.

ALIANZA NA KAMWAMBIE

Simulizi za kweli katika maisha yake ya mapenzi ndiyo zilifanya atambulike kwenye anga la Bongo Fleva. Nadhani unaukumbuka wimbo wake wa kwanza kabisa unaoitwa Kamwambie, ambao ulibeba historia ya kweli ya kutendwa na mwanamkie aliyempenda sana anayeitwa Sarah.

Ngoma hiyo ilimpa mafanikio katika mauzo ya albamu yake ya kwanza (Nenda Kamwambie) kufanya ashinde tuzo  za KTMA mwaka 2010 katika vipengele vitatu vya Msanii Bora Chipukizi, Wimbo Bora wa Mwaka na Wimbo Bora wa RnB.

Lakini pia wimbo huo ulimpa dili kubwa mbili ambazo ni ubalozi wa Malaria na kutumbuiza kwenye majukwaa ya siasa katika kampeni za urais za Jakaya Kikwete.

Lakini Diamond aliandika wimbo wake wa Mawazo baada ya kutendwa na Wolper, Moyo Wangu na Nataka Kulewa alimwimba Wema Sepetu na nyingine kama Mbagala, Ukimwona ziligusa ukweli wa maisha yake ya kuumizwa kimapenzi.

Diamond kutumia maudhui ya mapenzi yanayowahusu wapenzi wake wa zamani katika kuzidi kuiteka tasnia ya Bongo Fleva kwa vile nyimbo kama hizo ndiyo zimefanya leo hii awe msanii ghali zaidi Bongo.

SIKOMI

Ndani ya ngoma mpya ya Sikomi, Diamond wiki hii ameibua gumzo baada ya kuwataja waliowahi kuwa wapenzi wake, Wema Sepetu, Penny na Hamisa Mobetto.

Ngoma hii imepokewa kwa kishindo ambapo ndani ya saa 24 tayari ilikuwa imesikilizwa na watu zaidi ya laki tano ikiwa katika mfumo wa audio.

Katika vesi ya kwanza Diamond anasimulia jinsi alivyoukwaa ustaa na kujikuta mikononi mwa penzi la Wema Sepetu. Alimpenda Wema kiasi cha kuwa na wivu uliofanya agombane na mama yake, dada na washkaji zake.

Lakini Wema alimsaliti na kuwa na kigogo serikalini hali iliyofanya asiwaamini wasanii wa filamu kiasi cha kutoshangaa Sepetu kuhama CCM kwenda Chadema.

Baada ya hapo, alitia timu kwenye himaya na Vj Penny ambaye alimwambia ana mimba yake na yeye akamhonga gari lakini mrembo huyo akaichomoa.

Chibu hakuishia hapo ameweka wazi kuwa yeye ni mjinga kwa sababu licha ya Mungu kumtunuku Zari aliyemzaliwa watoto wawili, alimsaliti na Hamisa Mobetto.

NIACHE

Ni ngoma ya pili ambayo Diamond ameitoa wiki hii na ndani yake ameendelea kumzungumzia mmoja kati ya wapenzi wake wa zamani kwa mtindo wa mafumbo.

Diamond ameonyesha anamchukia huyo ex wake kiasi cha kutotaka hata kukutana naye hata kama kwenye mitandao ya kijamii huwa ana-like na kuposti picha zake.

HUWATUMIA KWENYE VIDEO

Baada ya kujua kuwa mahusiano yake huwa yanafutiliwa na watu wengi, Diamond toka kitambo aliamua kuwatumia wapenzi wake hao wa zamani.

Katika video ya Moyo Wangu, Diamond alimtumia ex wake Wema Sepetu. Video ya wimbo wake wa Mawazo aliwatumia  Jokate Mwegelo na Hamisa Mobetto ambaye amezaa naye,  pia Salome, alimtumia tena Mobetto.

Video zote hizo zinampa fedha kupitia mtandao wa YouTube kwa kuwa mpaka sasa zimetazamwa na watu zaidi ya milioni 3.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles