26 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

Masilahi duni kazini bado kikwazo- Ripoti

Na Salome Bruno (TUDARco), Mtanzania Digital

RIPOTI ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2020 imebaini kuwa Wafanyakazi katika Mikoa ya Manyara, Mtwara, Dar es Salaam na Mara wamelalamika kulipwa mishahara duni na waajiri wao kwenye baadhi ya makampuni.

Vijana wakiwa kazini kushusha mizigo kwenye gari.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imebainisha kuwa wafanyakazi hao wamelalamika kulipwa mishahara duni iliyoendelea kutolewa na baadhi ya makampuni hasa hotelini na viwandani na kwamba haiendani na gharama za maisha kwa sasa.

“Baadhi ya wafanyakazi waliohojiwa katika mikoa yote iliyotembelewa walilalamika kuhusu ucheleweshaji katika malipo ya mishahara. Kwa mfano, katika Mkoa wa Dar es Salaam baadhi ya wafanyakazi waliohojiwa walilalamika kuhusu mabadiliko ya mara kwa mara ya tarehe za kulipwa mishahara, suala ambalo ni kinyume na viwango vya       kazi.

“Aidha, tafiti zinaonesha kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka 2004 na mikataba mbalimbali inayohusiana na haki ya kufanya kazi, mfanyakazi ana haki ya kulipwa na mwajiri wake ujira wowote wa kifedha ambao mfanyakazi huyo anastahili,” imeeleza Ripoti hiyo na kuongeza kuwa;

“Sheria hii inatafsiri ujira kama “thamani kamili ya malipo katika fedha au vitu yanayofanywa au yanayodaiwa na mfanyakazi yanayotokana na ajira ya mfanyakazi huyo.” Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa haki ya kupata ujira stahiki na malipo ya haki (yanayolingana na kazi yake),” ameeleza ripoti hiyo.

Kwa mujibu wa LHRC, tafiti zinaonesha kuna changamoto kubwa hususan waraka wa serikali kuhusu viwango vya mishahara mwaka 2013 ambao ulitakiwa kufanyiwa marejeo kila baada ya miaka 3 lakini hadi sasa halijafanyika .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles