29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Ripoti: Corona ilivyoathiri biashara nchini

Na Judith Siaga (TUDARco), Mtanzania Digital

Kwa mujibu wa Ripoti iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) imeonyesha kuwa janga la corona liliathiri biashara kwa asilimia 50.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo

Ripoti hiyo inayofahamika kama Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara ya mwaka 2020 imeonyesha kuwa asilimia 97.9 ya wanachama wa shirikisho viwanda Tanzania (CTI) walikiri biashara zao kuathiriwa na janga la corona.

“Kwa mujibu wa utafiti ulifanywa na shirikisho la viwanda Tanzania CTI, Janga la corona lilileta athari kubwa katika mazingira ya biashara wakati   wa utafiti ambapo ilionyesha kwamba asilimia 97.9 ya wanachama wa shirikisho hilo walikiri kwamba biashara zao ziliathiriwa na janga hilo, ambapo zaidi ya sekta ndogo 4 kati ya 6 zilidai kupata hasara ya zaidi ya asilimia 50 ya mauzo.

“Aidha kwa upande wa upotezaji wa ajira asilimia 91 ya washiriki katika utafiti huo walitarajia kupunguza wafanyakazi.  Pia, tathmini ya athari ya kijamii na kiuchumi ya janga hilo chini, iliyofanywa na Mradi wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania inaonyesha kwamba corona iliathiri sekta na viwanda kadhaa, kama vile utalii na ukarimu, kilimo, biashara, na fedha,” imeeleza ripoti hiyo.

Ripoti imeongeza kuwa, katika utafiti wa biashara na haki za binadamu, karibia washiriki wote (95%) walikiri kwamba janga la corona liliathiri, uzalishaji, masoko na mauzo katika biashara zao, na kusababisha upunguzaji wa wafanyakazi mishahara na kutolipwa kabisa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles